Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

26 Septemba 2024

15:17:05
1488779

Netanyahu aogopa kwenda nje ya Israel kwa vipigo vya makombora vya Hizbullah

Ofisi ya waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni imetangaza kuakhirishwa tena safari ya Benjamin Netanyahu huko New York Marekani kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Uakhirishaji huo umekuja huku Hizbullah ya Lebanon ikiutwanga kwa mara ya kwanza kwa kombora la balestiki, mji mkuu wa Israel, Tel Aviv.

Gazeti la Times la utawala wa Kizayuni limeripoti kuwa, muda mfupi tu baada ya Hizbullah kuutwanga kwa makombora mji mkuu wa Israel kwa kutumia kombora la ardhi kwa ardhi. Gazeti hilo la Kizayuni pia limesema kuwa, Benjamin Netanyahu ameitisha kikao na taasisi za usalama kuhusu kuendelea mashambulizi nchini Lebanon au la.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Netanyahu ameakhirisha safari yake kuelekea New York baada ya Hizbullah kupanua wigo wa mashambulizi yake hadi katika mji mkuu wa utawala wa Kizayuni.

Leo Hizbullah ya Lebanon imesema kuwa, imeyatwanga kwa makombora maeneo mbalimbali ya Wazayuni ikiwa ni pamoja na kambi za siri za kijeshi za Wazayuni yakiwemo pia makao ya shirika la kijasusi la Israel MOSSAD katika viunga vya Tel Aviv.

Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetumia kombora la balestiki kupiga Tel Aviv ikiwa ni kwa mara ya kwanza, suala lililosababisha wahka mkubwa na ving'ora katika mji huo na maeneo mengine ya Israel ikiwa ni pamoja na Netanya.

Mfumo wa kuzuia makombora ya balestiki wa Israel wa Arrow ulizinduliwa mjini Tel Aviv mapema leo Jumatano, na kuwafanya wakazi wa mji huo kukimbilia mafichoni.

Hizbullah imetoa taarifa ikisema kuwa: "Katika kuunga mkono watu wetu wa Palestina huko Ukanda wa Gaza, na katika kuunga mkono Muqawama wao wa kishujaa na wa heshima, na katika kulinda Lebanon na watu wake, Muqawama wa Kiislamu (Hizbullah) umerusha kombora la balestiki la 'Qader 1' leo Jumatano, saa 6:30 asubuhi na kulenga makao makuu ya Mossad katika viunga vya Tel Aviv." 

Taarifa hiyo imeongeza kuwa: Makao makuu haya yanahusika na mauaji ya viongozi na uripuaji wa vifaa vya mawasiliano (pager na walkie-talkies) nchini Lebanon.

Hapo awali, Hizbullah ililenga kambi ya kijeshi ya Ilaniya ya Israel katika upande wa kaskazini wa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu kwa kutumia makombora ya Fadi-1.

342/