Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Waziri wa Mambo ya Nje na Naibu Waziri Mkuu wa Slovenia Tanja Fajon amesema, nchi yake inaunga mkono maamuzi ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel mfanya mauaji ya kimbari na kutoa wito wa kuwekewa vikwazo vya silaha utawala huo bandia.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Slovenia, ambaye kwa sasa ndiye Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika mwezi huu wa Septemba, ameeleza pia kwamba utegaji wa mada za miripuko uliofanywa na utawala bandia wa Israel kwenye vifaa vya mawasiliano vya pagers nchini Lebanon ni kitendo cha kigaidi.
Tanja Fajon ameashiria pia uamuzi wa hivi karibuni wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) iliyotangaza kuwa kukaliwa kwa mabavu kwa miaka 57 ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Gaza ni kinyume cha sheria na akabainisha kwamba, Israel lazima iondoke katika ardhi za Palestina inazozikalia kwa mabavu.
Taifa huru la Palestina hadi sasa limetambuliwa na zaidi ya nchi wanachama 140 wa Umoja wa Mataifa, ikiwa ni zaidi ya theluthi mbili ya wanachama wote wa umoja huo.
342/