Kiongozi wa Venezuela ametangaza mshikamano wa taifa lake na watu wa Gaza na Lebanon ambao amesema wamekuwa wahanga wa "mauaji ya kimbari" na "mashambulio ya kigaidi" ya utawala wa Israel unaoendeshwa na "muuaji ambaye anatukumbusha Hitler."
“Kwa niaba ya Kambi ya Kihistoria ya Mapinduzi, naeleza mshikamano wangu na watu wa Lebanon baada ya tangazo la kuuawa kiongozi wa Kiislamu, Sayyid Nasrullah", amesema Rais wa Venezuela.
"Waoga wa dunia wako kimya, lakini hakuna atakayenyamazisha wanamapinduzi," Maduro amesema katika mkutano wa watetezi wa Palestina huko La Guaira.
Rais wa Venezuela ametoa wito kwa Waislamu, Waarabu, na watu wengine kote duniani "kupaza sauti zao na kuonyesha mshikamano na watu wa Palestina, na watu wa Lebanon."
"Amri ya shambulio hilo ilitolewa kutoka makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York," amesema Nicolas Maduro, akimaanisha uwepo wa Netanyahu katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa wakati alipoidhinisha shambulio hilo la kigaidi.
Rais wa Cuba, Miguel Diaz-Canel pia amelaani mauaji yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya katibu Mkuu wa Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrallah.
342/