Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwangamizi wa watu Majabari.
﴿أَذِنَ لِلَّذِينَ يُقَاتَلُونَ بِأَنَّهُم ظُلِمُوا وَإِنَّ اللَّهَ عَلَى نَصْرِهِمْ لَقَدِيرٌ﴾
“Wameruhusiwa kupigana wale wanao pigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia (kuwapa ushindi)”. (Surat al-Hajj: Aya ya 39).
Baada ya yote, ukatili wa mnyama kichaa Israel kama vile kuua watoto, umemwaga sumu yake na kuufanya Ulimwengu wa Kiislamu wa Ummah wa Muhammad Rasulillah (s.a.w.w) kuomboleza msiba wake na kujeruhiwa moyo wake kwa kifo cha Kishahidi cha Sayyid Hassan Nasrullah.
Msimamo wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) baada ya kuuawa Shahidi Mjumbe Mashuhuri wa Jumuiya hii kuu, Sayyed Shahada wa upinzani, Bwana wa Mashahidi wa safu ya Muqawamah (Upinzani), Mpendwa »Sayyid Hasan Nasrullah«, si chochote ila ni kielelezo cha huzuni kubwa, na bila shaka kuonyesha huruma ya kina kwa watu wanaodhulumiwa wa Lebanon, na watu wanyonge (wasiokuwa na ulinzi) wa Palestina, na msisitizo juu ya maudhui haya muhimu sana:
Kuuawa Kishahidi kwa Bwana wa Mashahidi wa Upinzani (Muqawamah) - Sayyid Hasan Nasrullah - Haikuwa hali ya ajabu, kama vile mauaji ya mtangulizi wake, »Sayyid Abbas Mousawi«, Mwenyezi Mungu amrehemu, pia halikuwa jambo la ajabu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atupe Daraja za Mashahidi.
Mwisho mtamu wa njia ya Mujahidina na askari wa njia ya Mwenyezi Mungu na wale watu wanaoweka miguu yao katika vita dhidi ya dhulma na ukatili wa Marekani (Wanyama) walaji wa Ulimwengu, na Israel wanywa damu, ulikuwa wazi na bayana tangu mwanzo. Kimsingi, – Waumini – hao wanatafuta maisha ya (jihadi na) mapambano ili kufikia hamu yao ya kufa Kishahidi na Kijihadi.
﴿مِّنَ ٱلۡمُؤۡمِنِینَ رِجَالࣱ صَدَقُواْ مَا عَـٰهَدُواْ ٱللَّهَ عَلَیۡهِۖ فَمِنۡهُم مَّن قَضَىٰ نَحۡبَهُۥ وَمِنۡهُم مَّن یَنتَظِرُۖ وَمَا بَدَّلُواْ تَبۡدِیلࣰا﴾
“Miongoni mwa hawa Waumini wapo watu walio muahidi Mwenyezi Mungu kuwa watasimama imara na Mtume katika vita. Nao wakatimiza ahadi yao. Miongoni mwao wapo walio pata utukufu wa kufa Mashahidi, na wengine wamebakia wakiwa hai wakingojea nao kupata utukufu huo. Wala hawakuigeuza ahadi ya Mwenyezi Mungu waliyo jikatia juu ya nafsi yao, wala hawakugeuza chochote katika hayo.” (Surat Al-Ahzab: Aya ya 23).
Ijapokuwa mauaji ya kioga dhidi ya »Sayyid Hassan Nasrullah« yameacha pengo kubwa, na uharibifu usioweza kurekebishwa na maumivu makubwa kwa mwili na roho ya Hezbollah huko Lebanon na nyoyo za kila Muislamu mmoja mmoja duniani; lakini tunasisitiza bila kauli mbiu ya kwamba kila sehemu ya safu ya Upinzani (Muqawamah) ni kama mkondo unaotiririka, ambao bado uko hai, unaoongezeka, unaopanda na kufurika, na uliojaa matumaini ya kuzidi kuvikaribia vilele vya Nusra na Ushindi, ambavyo vinazidi kukaribia zaidi na zaidi, kadri ya Nusra na Ushindi kutoka kwa Mwenyezi Mungu unavyozidi kukaribia.
Moja ya mambo ya ajabu ambayo yanamshangaza kila mtu mwenye akili timamu na aliye huru bila aibu kabisa ni kitu kinachoitwa ‘Umoja wa Mataifa’, ambao badala ya kuweka (na kuthabitisha) amani, kumpa tanbihi mchokozi mwenye kuvuka mipaka, na kuheshimu haki halali ya ulinzi wa kujihami, unaidhinisha –Umoja huo – na kuidhinisha mauaji ya Watu wema (watendao mema na wanaorekebisha na kutengeneza).
Matokeo ya mawasiliano ya dhati na ya upendo kati ya Hezbollah ya Lebanon na Shule ya Kifikra ya viongozi wake wenye shani kubwa kuanzia "Imam Musa Sadr" hadi "Sayyid Hassan Nasrullah" na watu wote kwa ujumla wa Lebanon, kuanzia Mashia hadi Masunni, na kuanzia kwa Wakristo hadi Wayahudi, na kuanzia kwa walibrali hadi Wasekula (wasioamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu), mpaka kwa wana mapinduzi, wote kwa ujumla leo hii tunawaona wakiwa katika huzuni na maombolezo yasiyoelezeka, ambapo:
﴿إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَيَجْعَلُ لَهُمُ الرَّحْمَٰنُ وُدًّا﴾
“Hakika walio amini na wakatenda mema Arrahmani Mwingi wa Rehema atawajaalia mapenzi”. (Surat Maryam: Aya ya 96).
Historia itakumbuka daima jina la mtu mashuhuri kama «Sayyid Hasan Nasrullah» kuwa alikuwa ni Mujahid Mkubwa, Mshika Bendera wa Upinzani katika eneo (hili la Mashariki ya Kati), Mwanachuoni Mwenye maadili ya Kidini, Kiongozi na Mkurugenzi wa Kisiasa, Mwana Jihadi na Simba Shujaa, Kamanda katika uwanja wa vita, Mwanasayansi mwenye uhalisia, Kiongozi Mwadilifu na Shahidi aliyedhulumiwa; lakini akiwa ni imara na ambaye hayo yote yatadumu na kuandikwa katika kurasa za historia yake; basi na itambulike baya kuwa baada ya Nasrullah, sio mwisho wa njia yake, bali huo ni mwanzo wa Nasrullah (Ushindi na Nusra ya Mwenyezi Mungu), na kwa hakika tutapata nusra na ushindi wa Mwenyezi Mungu.
Mwisho: Kwa mujibu wa Amri na Fat’wa ya Kiwilayat ya Kiongozi Mwerevu wa watu huru, na Kiongozi wa Mashia Duniani, pamoja na Jumuiya za Ahlul-Bayt na washirika wa Jumuiya hii ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s), katika kuitikia Labbaika kwa amri na Fat’wa hiyo, tunasisitiza kufanya Jihadi dhidi ya adui wa Kizayuni na kukabiliana na utawala ghasibu na dhalimu na muovu, na kuwahurumia, kuwa pamoja nao, na kuwasaidia watu wanaokandamizwa na kudhulumiwa huko Lebanon na Palestina, na katika mipaka na maeneo mengine ya Kiislamu. Tunaona kuwa ni lazima na wajibu kwetu kupigana kwa suhula zote (tulizokuwa nazo) na kwa kila aina ya Jihad, ikiwemo Jihad kwa nafsi zetu, mali zetu, heshima yetu, elimu yetu, maarifa yetu, na sifa zetu.
﴿ وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنقَلَبٍ يَنقَلِبُونَ﴾
“Na wanao dhulumu watakuja jua ni mgeuko gani watakao geuka”
Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlulbayt(a.s)
29 Septemba, 2024