Main Title

source : Parstoday
Jumanne

1 Oktoba 2024

15:55:52
1490462

Madai ya Rais wa Marekani kuhusu kuwepo utulivu Asia Magharibi

Wakati utawala wa Kizayuni umeongeza wigo wa mivutano na vita huko Lebanon na Palestina; Rais Joe Biden wa Marekani amedai katika taarifa yake kwambe eti sasa wakati umefika kwa ajili ya kuwepo utulivu katika eneo la Asia Magharibi.

Amedai kuwa lengo kuu la Washington ni kupunguza mivutano na mizozo inayoendelea katika eneo kwa njia za kidiplomasia. Biden amedai kuwa: “Huko Gaza, tumejaribu kufikia makubaliano kwa msaada wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kuanzisha usitishaji vita na kuwaachia huru mateka wa Israel. Huko Lebanon pia tunajadiliana kuhusu makubaliano ambayo yatawarudisha wakaazi kutoka pande zote za mpaka kwenye makazi yao.”

Rais wa Marekani amedai kuwa: “Kwa kuidhinishwa makubaliano hayo, eneo zima la Asia Magharibi litapata utulivu mkubwa.” Matamshi hayo ya Biden yanakuja wakati ambao hatua za utawala wa Kizayuni hususan katika wiki iliyopita zimeongeza mivutano na taharuki katika eneo la Asia Magharibi. Jeshi la Kizayuni, ambalo limekuwa likizidisha vita dhidi ya Wapalestina wanaoishi Gaza kwa miezi kadhaa, pia lilifanya mashambulizi makubwa katika maeneo mbalimbali ya kusini mwa Lebanon wiki iliyopita.Katika kitendo cha jinai, Israel ililipua vifaa vya mawasiliano vya pager na walkie talkie za

maelfu ya Walebanon na vya wapiganaji  wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu na kusababisha mauaji ya makumi ya watu na kujeruhi zaidi ya watu elfu tatu. Kadhalika, katika siku chache zilizopita, utawala wa Kizayuni ulimuua kigaidi Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon Sayyid Nasrullah kwa kushambulia viunga vya kusini mwa Beirut na sasa unatayarisha mashambulizi ya nchi kavu dhidi ya nchi hiyo.


Biden amezungumzia utulivu katika eneo huku jinai za Israel zikiendelea kwa kuungwa mkono kikamilifu na Marekani na washirika wake. Marekani imekuwa muungaji mkono mkubwa wa utawala wa Kizayuni kwa miongo kadhaa sasa, ambapo jinai za Israel zimekuwa zikifanywa kwa uungaji mkono wa kijeshi na kisiasa kwa kupewa misaada ya kifedha ya Marekani kama ilivyokuwa katika vita vya Ghaza. Marekani imetenga mabilioni ya dola kama msaada wa kifedha na kijeshi kwa Israel. Hivi karibuni pia Marekani
imeipatia Israeli misaada ya makombora, ndege za kivita zisizo na rubani na ndege za kivita aina ya F-35 za kizazi cha tano na hivyo kuandaa mazingira ya kuendelea uchokozi wa Netanyahu dhidi ya mataifa ya eneo.


Hivi sasa, kufuatia kupanuka hujuma ya Israel dhidi ya Lebanon na kuuawa shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, Rais wa Marekani sanjari na kuunga mkono hatua hiyo ya utawala wa Kizayuni, amekitaja kitendo cha kuuawa shahidi Sayyid Nasrallah kuwa eti ni utekelezaji wa haki. Utawala wa Biden umekuwa chini ya mashinikizo kwa muda mrefu. Maoni ya umma ya ndani na ya kimataifa yanataka Marekani ishinikize usitishaji vita na kufikiwa makubaliano ya usitisha vita huko Gaza, lakini serikali ya nchi hiyo imekuwa na misimamo mingi  inayokinzana kuhusu kadhia hii na
hatimaye kutekeleza maslahi na matakwa ya Israeli jambo ambalo limepelekea waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni kuendeleza jinai zake katika eneo bila woga wowote.
Wakati Rais wa Marekani anaitaja hali ya sasa kuwa ni wakati wa usitishaji vita, hasira za wananchi dhidi ya hatua za Israel zimeongezeka zaidi, ambapo nchi tofauti zimeonyesha hisia tofauti kwa jinai za Israel, hususan mauaji ya Sayyid Hassan Nasrullah. Kwa hakika, kuongezeka mvutano katika eneo hilo kumepelekea kuongezeka wasiwasi katika ngazi za kimataifa.

Katika muktadha huu, Josep Borrell, mkuu wa siasa za kigeni katika Umoja wa Ulaya, amesema: “Tunaenda kwenye vita virefu.” Jarida la Economist pia limeandika katika muktadha huu: 'Shambulio dhidi ya makao makuu ya kamandi kuu ya Hizbullah huko Beirut limethibitisha kuwa Netanyahu hataki usitishaji mapigano kwani shambulio hili lenyewe linaweza kubatilisha mpango wowote wa usitishaji vita, kwa sababu ni ishara kuwa Israel inazidisha taharuki. Katika hali hii Rais wa Marekani amedai kuwa eti
kuna utulivu katika eneo la Asia Magharibi.'

342/