Main Title

source : Parstoday
Jumatano

2 Oktoba 2024

20:05:16
1491052

Makundi ya Muqawama yaishukuru na kuipongeza Iran kwa kutekeleza Operesheni Ahadi ya Kweli 2

Makundi ya Muqawama yamepongeza jibu kali lililotolewa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa utawala wa Kizayuni kufuatia Operesheni Ahadi ya Kweli 2 na kutekelezwa kwa mafanikio shambulio la makombora la Iran katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na kulenga shabaha zilizokusudiwa kwa asilimia 90 ya makombora yaliyorushwa na vikosi vya ulinzi vya Iran.

Taarifa iliyotolewa na Kamati za Muqawama za Wananchi wa Palestina mbali na kupongeza operesheni iliyotekelezwa kwa mafanikio ya Ahadi ya Kweli 2, imeeleza kwamba: shambulio la Iran na woga na kuchanganyikiwa kulioupata utawala ghasibu na hofu iliyozijaa nyoyo za walowezi na viongozi wao yanadhihirisha udhaifu mkubwa na utete wa mfumo wa Kizayuni.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo, imebainishwa kuwa, shambulio la makombora la Iran dhidi ya Israel ni sehemu ya kisasi cha haki ambacho inapasa kitekelezwe kwa wahalifu wa Kizayuni na waungaji mkono wao katika serikali ya watenda jinai wa Marekani na kuongeza kuwa: majibu ya Iran yanaonyesha kuwa katika hatua mpya ya makabiliano, Muqawama uko tayari na uko imara na umeingia kwenye awamu mpya kwa ajili ya kulipiza kisasi cha damu za viongozi wao Mashahidi na raia waso na uinzi

Wakati huo huo, harakati ya Intifadha ya Fat-h imeeleza katika taarifa yake kwamba, jibu la Iran ni hatua ya kihistoria ya mabadiliko katika mwenendo wa mzozo na adui Mzayuni, na hilo lilikuwa jibu la kawaida na la kutarajiwa kwa jinai za adui Mzayuni yakiwemo mauaji aliyofanya ya kumuuua Shahidi Ismail Haniyeh na Shahidi Seyed Hassan Nasrullah na viongozi wote waliouawa shahidi.../

342/