Main Title

source : Abna
Jumamosi

5 Oktoba 2024

19:58:10
1491881

Dua ya Khitma kwa Roho ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah imefanyika Leo hii Jijini Dar-es-Salam - Tanzania.

Kitengo cha Utamaduni cha Iran - Dar-es-salaam, Tanzania kimefanya Dua Maalum, Khitma na Visomo kadhaa katika Mnasaba wa Kuomboleza na kumtakia Rehma na Radhi za Allah, Kiongozi Mshika Bendera wa Muqawamah, Mtetezi Haki, Utu, Heshima na Uadilifu kwa Wapalestina na Walebanon, Sayyid Hassan Nasrullah.

Aliyeuliwa Kishahidi na Kidhulma katika Shambulizi la Kigaidi la Kizayuni Kusini mwa Lebanon.

Hajat Fatima Mwiru - Mwenyekiti wa Wanawake wa T.I.C _ TAIFA

Alipata fursa ya kuhutubia katika hadhara hii na kuongelea sehemu ya Sifa na Shakhsia ya Sayyid Hassan Nasrullah.

Miongoni mwa shakhsia kadhaa zilizohudhuria katika Majlis hii:

1_Balozi wa Iran Nchini Tanzania, Mheshimiwa Hussein Al-Vandi.

2_Dr.Khatibu.

3_Sheikh A.Kwezi.

4_Sheikh Ghawthi.

5_Askofu kutoka Kilosa.

6-Na wengine wengi.

Mwenyezi Mungu Amrehemu Bwana wa Mashahidi wa Muqawamah - Sayyid Hassan Nasrullah.