Main Title

source : Abna
Jumatatu

7 Oktoba 2024

18:27:41
1492541

Msomi Mashuhuri wa Pakistan: Mapinduzi ya Kiislamu ni "Mti Mzuri" (Al_Shajarat Al_Tayyibat) na Hezbollah ni "Tawi la Mtu huo"

Mkurugenzi wa Seminari (Hawzat) ya 'Jumuiya ya Ur'wat al-Wuthqa' ya Pakistan aliielezea Hezbollah kama "Tawi la Mti huu Mzuri" na akasema: Jaribio la kuharibu (na kupoteza) matunda ya Mti huu Mzuri kwa Kufa Kishahidi kwa Viongozi wa Upinzani halitaleta pengo lolote katika Safu ya Upinzani.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul_Bayt (a.s) -ABNA- Hojjat al-Islam wal-Muslimina, Sayyid Javad Naqvi, Mkurugenzi wa Seminari (Hawzat) ya Jumuiya ya Ur'wat al-Wuthqa', alisema:

Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yamethibitisha kuwa ni "Mti Mzuri" ambao (waovu wa) Dunia nzima wametumia juhudi zao zote kuumaliza (lakini wameshindwa).

Aliielezea Hezbollah kuwa ni "Tawi la "Mti huu Mzuri" na akasema:

Kujaribu kuharibu (na kuyapoteza) "Matunda ya Mti huu Mzuri" kwa kuuawa Kishahidi kwa Viongozi wa Upinzani kamwe hakuwezi kuleta pengo lolote katika Safu ya Upinzani. Shahadat ni sehemu ya njia hii inayofanya njia iwe wazi na bayana zaidi.

Mwanazuoni huyo Mashuhuri wa Pakistan amesema:

Leo hii, idadi kubwa ya Waislamu wanateseka kutokana na ukosefu wa utulivu, kukosa uthabiti na kudhalilishwa licha ya utajiri mkubwa waliokuwa nao.

Aina hii ya maisha ni kama 'Mti ambao (shina au) msingi wake hauna nguvu na mizizi yake ni dhaifu na umekatwa kutokea juu.

Sayyid Jawad Naqvi alisema zaidi kuwa:

Tofauti kati ya "Tabaka nzuri na Tabaka mbaya" ilidhihirika wazi katika vita vya Gaza. Leo hii, wale watu walio chagua kuwa kimya kuhusu vita vya Gaza; wanaainishwa kuwa ni watu wa upande wa shari na makhabithi.