Main Title

source : Abna
Jumanne

8 Oktoba 2024

16:14:22
1492848

Maoni muhimu kuhusu Khutba ya Swala ya Ijumaa ya Kiongozi wa Mapinduzi kutoka miongoni mwa Masunni

Mwanafikra mashuhuri wa Yemen alisema: Watu wengi katika Ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu walishangazwa na ufasaha na Hotuba ya Ayatollah Khamenei kwa Lugha ya Kiarabu. Mwenyezi Mungu alitaka sifa fulani za Kiongozi wa Mapinduzi zijulikane.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Ingawa ni siku chache sasa zimepita tangu Ayatollah Khamenei aongoze Swala ya Ijumaa ya Ushindi na kutoa hotuba zake muhimu katika jumla ya Khutba mbili za Swala ya Ijumaa moja ikiwa ni kwa lugha ya Kiajemi na ya pili ikiwa ni kwa lugha ya Kiarabu, nukta muhimu za Khutba hizi mbili na matokeo yake na athari zake vinazidi kuonekana katika jamii tofauti tofauti za walimwengu, ikiwa ni pamoja na Waislamu wa Shia na Sunni.

 

 

"Essam al-Emad", Mwanafikra wa Yemen na mmoja wa Wanazuoni wa Seminari (Hawzat) ya Qom, katika mazungumzo na mwandishi ABNA, alijadili juu ya (uhusiano au) uwiano uliopo kati ya mtazamo wa Kiongozi wa Mapinduzi mkabala wa Qur'an Tukufu, na athari ya Khutba yake katika Swala ya "Ijumaa ya Ushindi" kwa Ahlu Sunna wote Ulimwenguni, ambapo andiko la mazungumzo hayo ni kama ifuatavyo hapo chini:

 

 

ABNA: Tafadhali toa maoni yako kuhusiana na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kuongoza Swala ya Ijumaa ya Ushindi, na kusoma (kutoa) Khutba ya pili kwa Lugha ya Kiarabu kwa ufasaha wake.

 

 

Kwa maoni yangu, Qur'an Tukufu ndiyo siri ya Shakhsia ya Ayatollah Khamenei na ufunguo wa urithi wake mkuu katika Tauhidi na Sayansi (Elimu na Maarifa). Mwenyezi Mungu anaeleza mawazo na matendo yake yote kupitia Qur'an Tukufu, na siri ya mafanikio ya Kiongozi wa Mapinduzi ilikuwa ni kuwatetea wanyonge huko Palestina, Lebanon na Yemen kwa kuzingatia muongozo na maelekezo ya Qur'an Tukufu.

 

Roho ya Qur’an ya Hazrat Ayatollah Khamenei ilidhihirika kupitia kutafsiri (kutarjumu) kwake kitabu cha Shahidi Sayyid Qutb katika Kivuli cha Qur’an Tukufu kutoka lugha ya Kiarabu hadi lugha Kiajemi. Tafsiri hii ya kitabu hichoKilifanywa na kiongozi wa Mapinduzi katika umri wa ujana wake. Kilichomsaidia katika kuifahamu na kuifasiri Qur’an Tukufu ni kwamba alijifunza lugha ya Qur’an kutoka kwa Mama yake ambaye alikuwa akijua vizuri Kiarabu na alikuwa mjuzi wa kusoma Qur’an Tukufu.

 

Mapenzi makubwa ya Ayatollah Khamenei kwa Qur'an Tukufu yalimfanya kuwa makini na lugha ya Kiarabu. Yeyote anayesoma mashairi yake kwa lugha ya Kiarabu anaelewa kwamba ushairi wake wa Kiarabu ni bora kuliko ushairi wa washairi wa kisasa wa Kiarabu, au mtu yeyote anayeelewa undani wa maoni ya Ayatollah Khamenei kuhusu kitabu kigumu zaidi cha fasihi ya Kiarabu kiitwacho

 - كِتابُ الأغاني، أَبو الفَرَجِ اِصفَهاني (ولد ۲۸۴هـ.ق- توفي ۳۵۶هـ.ق - (Kitab al-Agha’niy, cha Abul Faraj Isfahani / ambaye alizaliwa mwaka: 897 AD, Isfahan, na akafariki Tarehe: 20 Novemba, 967AD akiwa na umri wa miaka 70, na alizikwa Baghdad, Iraq) ... Anaelewa kabisa kuwa yeye ni mtaalamu wa mashairi ya Kiarabu.

 

Haya yote yanaonyesha mapenzi na mahaba ya Ayatollah Khamenei aliyokuwa nayo kwa Qur’anTukufu. Na unapokaa naye, unagundua kabisa kwamba Kiongozi huyu wa Mapinduzi anazungumza nawe kwa Kiarabu safi na fasaha. Kwa hiyo, (katika Swala ya Ijumaa ya Ushindi) tuliona kwamba Ayatollah Khamenei ametoa Khutba safi ya Ijumaa kwa lugha ya Kiarabu fasaha.

 

Hazrat Ayatollah Khamenei alitafsiri (alitarjumu) Kitabu cha Sayyid Qutb kuhusiana na Tafsiri ya Qur’an Tukufu kutoka Lugha ya Kiarabu hadi Lugha ya Kiajemi.

 

Nikiwa kama Muwahabi wa zamani, haikuwahi kuniingia akilini kwamba Sayyid Ali Khamenei ametafsiri (ametarjumu) Kitabu cha Sayyid Qutb juu ya Tafsiri ya Qur’an Tukufu, na haikunijia akilini kabisa kwamba Sayyid ana elimu na maarifa hayo ya kipekee juu ya Mwenyezi Mungu na Tauhidi, na haikutokea kuniingia akilini kwamba Hazrat Ayatollah Khamenei amefanye utafiti kama huo juu ya matukio ya Siku ya Kiyama ndani ya Qur'an Tukufu. Na haikuwahi pia kuniingia akilini kwamba ushairi wa Kiongozi wa Mapinduzi kwa Lugha ya Kiarabu ni bora zaidi kuliko ushairi wa washairi wa Kiarabu katika zama zetu za leo, na sikudhani kabisa (wala kuwahi kufikiri) kwamba yeye ndiye wa pekee mwenye kuwahami na kuwatetea Masunni wa huko Gaza na Ukingo wa Magharibi.

 

 

Hakika Mwenyezi Mungu alitaka maneno ya Ayatollah Khamenei aliyohutubia umati mkubwa wa watu kwa lugha ya Kiarabu fasaha Siku ya Ijumaa ya Ushindi yafike kwenye masikio ya Walimwengu wote, ili Ushahidi ukamilike kwa kila mtu.

 

 

ABNA: Ni mwitikio upi uliopo miongoni mwa Jamii ya Masunni kuhusiana na Khutba ya ya pili ya Ayatollah Khamenei liyoitoa kwa lugha ya Kiarabu katika Swala ya Ijumaa ya Ushindi?.

 

 

Watu wengi katika Ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu walishangazwa na ufasaha na hotuba ya Ayatollah Khamenei kwa lugha ya Kiarabu. Mwenyezi Mungu alitaka (Siku hiyo ya Swala ya Ijumaa ya Ushindi) sifa fulani za Kiongozi wa Mapinduzi zijulikane kwa Walimwengu wote.

 

Mmoja wa Masunni wa Misri alisema: Naapa kwa Mwenyezi Mungu, baada ya kusikia maneno ya Ayatollah Khamenei katika Khutba ya Swala ya Ijumaa, mtazamo wangu kuhusu Iran umebadilika kwa zaidi ya digrii (daraja) milioni moja.

 

Pia, mmoja wa watu wa Jamii ya Kisunni wa Tunisia alisema: Mwenyezi Mungu awalaani wale waliotupotosha na kuitambulisha Iran kuwa ni adui mkubwa, lakini kwa Hotuba ya Ayatollah Khamenei, mtazamo wangu kuhusu Iran umebadilika.

 

Raia mmoja wa Jamii ya Kisunni wa Morocco alisema: Khutba zote za Swala ya Ijumaa nchini Saudi Arabia ni kwa ajili ya kumsifu Mwana Mfalme Mohammed bin Salman, ambaye jambo muhimu na la pekee kwake ni kufanya sherehe (hafla) za kudansi na muziki, lakini katika Khutba ya Swala ya Ijumaa ya Hazrat Ayatollah Khamenei, sikuona chochote isipokuwa uwezo wake na ujasiri wake dhidi ya vitisho vya Amerika na Israeli, na hilo lilionekana wazi kwa kila mtu.

 

Mmoja wa Masunni wa Jordan alisema kwamba: Ayatollah Khamenei anazungumza Kiarabu vizuri zaidi kuliko watawala wahaini wa Kiarabu.

 

Mpalestina mmoja wa Jamii ya Kisunni pia alisema: Khutba ya Ayatollah Khamenei ndiyo Khutba pekee ya Ijumaa ambayo haikutolewa chini ya usimamizi (na udhibiti) wa watawala mafisadi.

 

Pia, raia mmoja wa Kisunni wa Algeria alisisitiza akisema: Enyi wasaliti wa Kiarabu, je hamumuoni haya kwa Imam Sayyid Ali Khamenei Al-Hashemi?!. Raia mwingine wa Kisunni kutoka Lebanon baada ya kusikiliza Khutba ya Ayatollah Khamenei kuhusu ulazima wa kuwepo “Umoja baina ya Sunni na Shia” alisema: Iran imefanikiwa kuunda “Umoja kati ya Sunni na Shia” baada ya juhudi za Saudi Arabia za kuleta mgawanyiko kati ya Sunni na Shia.

Mmoja wa watu wa Jamii ya Kisunni wa Mauritania pia amesema: Swala ya Ijumaa iliyoongozwa na Imam Khamenei ni Swala ya Ijumaa pekee ambayo haihitaji idhini ya Marekani.

Mwisho napenda kumuomba Mwenyezi Mungu azidi kumuweka Kiongozi huyu mkubwa chini ya hifadhi na ulinzi Wake, na anijaalie kuwa miongoni mwa wanaojumuishwa katika dua na maombi yake.