Kwa mujibu wa ripoti hii, tarehe 27 Septemba 2024, mashambulizi makubwa ya anga ya utawala wa Kizayuni katika viunga vya Kusini mwa Mji wa Beirut yalisababisha milipuko mikubwa na idadi kubwa ya raia wa Lebanon kuuawa Shahidi katika mashambulizi hayo, miongoni mwa Mashahidi hao ni Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hezbollah ya Lebanon.
Kufuatia tukio hilo, Bahrain ilishuhudia kushadidishwa ukandamizaji dhidi ya uhuru wa kujieleza na mikusanyiko ya amani kunakofanywa na mamlaka za utawala wa Aali - Khalifa ambazo zilichukua hatua kali dhidi ya raia wa Bahrain waliotoa maoni na misimamo yao kuhusiana na mauaji hayo ya kigaidi nay a kioga ya kizayuni.
Tangu wakati huo, takriban raia 100 wa Bahrain wamekamatwa au kuitwa (ili kuhojiwa) kwa kushiriki katika maandamano ya amani au kutoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mauaji ya Sayyid Hassan Nasrullah, na baadhi yao walitambulishwa kwenye Kitengo cha Uhalifu wa Mtandaoni cha Upelelezi wa Jinai na kulazimishwa kufuta machapisho yao yaliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii, pia kwa baadhi ya watu hao, kesi ya kimahakama ilifunguliwa na kesi yao kupelekwa kwenye Ofisi ya Mwendesha Mashitaka kwa ajili ya kufanyiwa kazi.
Miongoni mwa waliozuiliwa ni watu wanne Mashuhuri wa Kidini wa jamii ya Bahrain, akiwemo Hojjat al-Islami wal-Muslimina, Sayyid Majid Mash’al, Mkuu wa Baraza la Wanazuoni wa Bahrain, na Hojjat al-Islami wal- Muslimina, Fadhil al-Zaki, Mkuu wa Kamati ya Sharia wa Baraza hili.