Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Ndege za kivita za utawala haram wa Kizayuni zilifanya jinai nyingine ya kutisha dhidi ya Wananchi madhulumu wa Palestina siku ya Jumatano.
Mara hii Wazayuni hao wavamizi hawakuziacha hata familia zilizopoteza makazi yao katika eneo la Al-Mawasi huko Khan Yunis na walichofanya ni kuzishambulia kwa mabomu kwa njia ya kikatili na ya kutisha.
Wavamizi wa Kizayuni hapo awali walikuwa wamelitangaza eneo hili kuwa ni eneo salama.