Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul_Bayt (a.s) - ABNA - Vyanzo vya Habari vimetangaza juu ya hali ya hivi karibuni ya Madhabahu / Haram Tukufu ya Hadhrat Zainab (s.a) na usalama wake.
Kwa mujibu wa ripoti hii, Madhabahu ya Hadhrat Zainab (a.s) bado yamefungwa kwa Mazuwwari kutokana na hali ya sasa ya Syria, lakini Madhabahu / Haram ya Bibi huyo Mtukufu imefunguliwa tena kwa ajili ya Mazuwwari na watumishi wa Haram hii ya Hadhrat Zainab (s.a) kwa ajili ya kusafisha sehemu mbalimbali za Madhabahu / Haram na kuwakaribisha Mazuwwari.
Vile vile, kwa kuendelea kuimarika kwa hali ya usalama katika eneo la Zainabiyah la Damascus na kufunguliwa Haram / Madhabahu Tukufu ya Hazrat Zainab (s.a) kwa kwa ajili ya Mazuwwari, Sala za Jamaa zilianza tena katika Haram hii Tukufu kwa kuhudhuriwa na Mashia wa eneo hili.