Imeelezwa katika taarifa hii kama ifuatavyo: Tunapenda kuwafahamisha Wapenzi wa Haram Tukufu ya Hadhrat Ruqayyah (amani iwe juu yake) kwamba wajumbe kutoka kundi la Tahrir al-Sham walitembelea Haram hiyo Tukufu kwa kuchunga heshima kamili, adabu na desturi za Kiislamu, na kisha kuondoka kwenye Haram hiyo baada ya muda saa moja.
Inafaa kuashiria kuwa katika Harakati za kubadilisha Serikali ya Syria na kuchukua Madaraka ya Kundi la Tahrir al-Sham katika nchi hii, hapakuwa na uvamizi wowote kwenye Madhabahu / Haram ya Hadhrat Ruqayyah (s.a) na eneo hili Tukufu liko katika usalama kamili katikati mwa Mji wa Damascus.