Main Title

source : Abna
Jumatatu

16 Desemba 2024

18:43:15
1514239

Picha za kutisha za mtoto wa Kipalestina aliyepoteza miguu miwili na mkono mmoja

Kuchapishwa kwa picha za mtoto wa Kipalestina aliyepoteza miguu miwili na mkono kutokana na mashambulizi ya Israel, kuliibua hisia na uzingatiaji wa watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (a.s) - ABNA - Zimechapishwa picha za mtoto wa Kipalestina aliyepoteza miguu miwili na mkono mmoja kutokana na mashambulizi ya Israel, ambapo ziliibua hisia na uzingatiaji wa watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa UNICEF, tangu kuanza kwa vita kati ya Hamas na jeshi la Israel hadi Septemba 2024, zaidi ya watoto 70 huko Gaza wanakabiliwa na majeraha mabaya na ulemavu kila siku.

AFP iliripoti Jumamosi, 14 Disemba, ikinukuu Wizara ya Afya ya Gaza ilisema, kwamba watu wasiopungua 44,930 wameuawa katika kipindi cha miezi 14 iliyopita.

UNICEF pia ilitangaza katika ripoti yake kwamba zaidi ya watoto 10,000 na watu wazima wanapotea chini ya vifusi vya majengo yaliyoharibiwa huko Gaza, na maelfu ya watoto wamepoteza kiungo kimoja au viwili katika miezi mitatu ya kwanza ya vita.

Shirika la Afya Ulimwenguni linakadiria kuwa zaidi ya 22,500 ya wale waliojeruhiwa walipata "majeraha ya kubadilisha maisha" na wanahitaji huduma za ukarabati kwa "sasa na kwa miaka ijayo."