Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul Bayt (a.s) - ABNA - Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa Kombora la Balistiki lililorushwa kutoka katika ardhi ya Yemen liliupiga mji wa Tel Aviv, Mji Mkuu wa utawala Haram wa Kizayuni.
Jeshi la Kizayuni pia limekiri kwa kutoa taarifa kwamba kombora hilo lililorushwa na Wayemeni liliupiga mji wa Tel Aviv baada ya kupita kwenye mfumo wa ulinzi wa Iron Dome.
Vyombo vya Habari vya Kiebrania vilikiri kwamba takriban Wazayuni watano walijeruhiwa katika shambulio hili la Kombora la Balistiki, na uharibifu mkubwa ulifanyika kwenye majengo karibu na mahali ambapo roketi lilipiga.