Main Title

source : Abna
Jumatano

8 Januari 2025

18:53:53
1521300

Ayatullah Khamenei: Marekani daima imekuwa ikifanya makosa katika mtazamo wake dhidi ya Iran

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema kuwa, Marekani mara zote imekuwa ikifanya makosa katika mtazamo wake dhidi ya Iran kwa miongo kadhaa sasa.

Ayatullah Khamenei amesema hayo Jumatano alipokutana na wananchi wa mji wa Qom wa kusini mwa Tehran kwa mnasaba wa kukumbuka harakati ya Januari 9, 1978 iliyofanywa na wananchi wa Qom kwa ajili ya kumuunga mkono muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu, Imam Ruhullah Khomeini na kusaidia kufikiwa ushindi kamili wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran mwaka 1979.

Katika sehemu moja ya miongozo yake iliyojaa busara, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: "Chini ya [utawala wa kiimla wa zamani wa Iran wa ufalme wa] Pahlavi, Iran ilitumika kama ngome ya kufanikisha maslahi ya Marekani."

Aidha amesema: "Baada ya Mapinduzi, Wamarekani wamekuwa wakifanya makosa mengi kuhusu Iran kwa miongo kadhaa sasa."

Imam Khamenei amefafanua zaidi kwa kusema kuwa, matamshi yake hayo yanawalenga zaidi wale "wanaotishwa na makeke ya Marekani."

Amma kuhusiana na utawala wa Kizayuni, Ayatullah Khamenei amesema kuwa, mtu asidhani kwamba Marekani na utawala wa Kizayuni hivi sasa wamebadilika na wako tofauti na walivyokuwa zamani, hapana, hawajabadilika. Tunapaswa kuwa macho zaidi kwa maelfu ya mara hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote. 

Matamshi ya Ayatullah Khamenei yalikuwa na maana ya kujibu maswali yaliyoulizwa na baadhi ya watu kuhusu kwa nini Iran inafanya mazungumzo na nchi za Ulaya lakini haiko tayari kuingia katika mazungumzo na Marekani.

Wachambuzi wa mambo wanayataja Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran kuwa ni nguvu iliyozalisha harakati ya kimataifa dhidi ya ukoloni katika ngazi ya juu zaidi na kwamba Marekani inaendelea kupata hasara kubwa kutokana na misimamo imara ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Chanzo: IQNA