Luqman mwenye hekim alisema:
Ewe mwanangu! Allah swt huuisha nyoyo za watu kwa nuru ya elimu kama vile anavyohuisha ardhi iliyokufa kwa baraka za mvua kutokea mbinguni. (Bihar al-Anwaar: Jz. 1)
Maelezo mafupi:
Moyo wa mtu kama ardhi sawa na bustani ambapo kila ya aina ya mimea, mbegu za maua, miche na miti imara huwa imeenea kila mahala, na lau itapatiwa maji kwa wakati wake, basi bustani hiyo itashamiri na kupendeza mno. Kwa hakika umwagiliaji wa bustani hiyo ya mioyo yetu huhitaji matone ya mvua ya sayansi na elimu. Hivyo nyoyo ambazo hazina elimu huwa zimekufa, zisizo na nuru wala mazao yoyote. Inatubidi sisi daima tuhuishe nyoyo zetu kwa nuru ya elimu.
Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho "MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA" - Ayatullah Makarim Shirazi