Main Title

source : Abna
Alhamisi

9 Januari 2025

20:25:46
1521634

Takwimu za kutisha kutoka Gaza baada ya siku 460 za vita vya uharibifu vya Wavamizi Wazayuni

Utawala wa Kizayuni kwa uungwaji mkono wa Marekani na Ulaya na vile vile Uingereza unapuuza maazimio 2 ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya kusimamisha mara moja mashambulizi yake dhidi ya Ukanda wa Gaza na pia maagizo ya Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu kuhusu haja hiyo kusimamisha vita hiyo na kuchukua hatua za kuzuia mauaji ya kimbari na kujaribu kuboresha hali ya Kibinadamu huko Gaza.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - ABNA - Tarehe 8 Januari 2025, baada ya siku 460 tangu kuanza kwa vita vya mauaji ya kimbari ya utawala ghasibu dhidi ya Ukanda wa Gaza, Ofisi ya vyombo vya Habari ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina ilitoa taarifa na kutangaza takwimu muhimu zaidi zinazohusiana na vita hivi.

Katika ripoti yake, taasisi hii ya Palestina ilieleza takwimu za hivi punde kuhusiana na vita hivi vya uharibifu, ambazo unaweza kuziona hapa chini kama ifuatavyo:

- Siku 460 za vita vya mauaji ya halaiki dhidi ya Gaza.

- Jinai 10,015 zilizofanywa kwa ujumla na jeshi Vamizi la Kizayuni.

- Jinai 7,182 zilizofanywa na wavamizi wa Kizayuni dhidi ya familia za Wapalestina.

- Familia 1,600 ziliharibiwa kabisa, ambapo idadi yao ilikuwa watu 5,612.

- Familia 3,471 za Wapalestina, ni mmoja tu kati yao aliyebaki hai, na idadi ya Mashahidi wa familia hizi ilikuwa ni watu 9,000.

- 57,136 wamekuwa Mashahidi na waliopotea..

- Watu 11,200 waliopotea ambao miili yao bado haijasajiliwa Hospitalini.

- Mashahidi 45,936 ambao wamesajiliwa rasmi Hospitalini.

- Watoto 17,841 waliouawa Kishahidi.

- Watoto 240 waliouawa Kishahidi baada ya kuzaliwa katika vita vya mauaji ya kimbari.

- Watoto 858 walio chini ya mwaka mmoja waliouawa katika vita hivi.

- Mashahidi 44 waliouawa kutokana na utapiamlo.

- Mashahidi 8 waliouawa kwa sababu ya baridi kali, 7 kati yao walikuwa watoto.

- Mashahidi 12,298 Wanawake.

- Mashahidi 1,668 kutoka kwa wafanyakazi wa matibabu.

- Mashahidi 94 kutoka idara ya ulinzi wa raia.

- Mashahidi 202 Wanahabari.

- Mashahidi 736 kutoka kwa vikosi vya Polisi ambao walifanya kazi kwa ajili ya usalama wa misaada ya kibinadamu.

- 149 Kwa kulenga vikosi vya Polisi vilivyofanya kazi kwa ajili ya usalama wa misaada ya kibinadamu.

- Makaburi 7 ya halaiki yaliyoundwa na Jeshi vamizi la Kizayuni katika Hospitali.

- Mashahidi 520 waliondolewa kutoka kwenye makaburi 7 ya halaiki katika Hospitali.

- Watu 109,274 walijeruhiwa ambao walikwenda Hospitalini (kupata matibabu).

- 399 ni walijeruhiwa waandishi na wana habari.

- 70% ya waliojeruhiwa walikuwa watoto na wanawake.

- Vituo 218 vya makazi ya wakimbizi vilivyolengwa na wavamizi wa kizayuni.

Asilimia 10 ya maeneo ya Ukanda wa Gaza yameteuliwa kuwa maeneo ya kibinadamu na wavamizi.

- Watoto 35,074 wamebakia bila wazazi Baba na Mama au mmoja wao.

- Wanawake 12,132 waliopoteza waume zao.

- Watoto 3,500 wako katika hatari ya kifo kutokana na utapiamlo na ukosefu wa dawa.

- Siku 246 za kizuizi cha kivuko cha mwisho cha Gaza kulichowekwa na wavamizi wa kizayuni.

- Majeruhi 12,600 wanaohitaji kuondoka Gaza kwa ajili ya matibabu.

- Wagonjwa 12,500 wa saratani ambao wanapaswa kuondoka Gaza ili kuendelea na matibabu yao.

- Wagonjwa 3,000 tofauti wanaohitaji kuondoka Gaza kwa ajili ya matibabu zaidi.

- Kesi 2,136,026 za magonjwa ya kuambukiza kwa sababu ya kuhama (kuhamasishwa na kuwa wakimbizi).

- Kesi 71,338 za hepatitis C kwa sababu ya kuhama (Kuhamasishwa na kufanywa Wakimbizi).

- Wajawazito 60,000 ambao wako hatarini kutokana na ukosefu wa usafi.

- Wagonjwa 350,000 wa muda mrefu wako hatarini kutokana na ukosefu wa dawa.

- Wafungwa 6,600 kutoka Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa mauaji ya kimbari ya uvamizi huo wa Kizayuni.

- 331 Ni wafanyakazi wa matibabu (madaktari) waliokamatwa, ambapo 3 kati yao waliuawa gerezani.

- Kukamatwa kwa watu 43 ambao ni waandishi wa habari na ambao utambulisho wao umebainishwa.

- Kesi 26 za kukamatwa kwa vikosi vya ulinzi wa raia.

- Watu 2,000,000 waliokimbia makazi yao katika Ukanda wa Gaza.

 Mahema 11,000 yamejengwa, lakini wakati huo huo, hayafai kwa waliohamishwa (na kutolewa kwenye makazi yao).

- Majengo 214 ya Serikali yameharibiwa katika mashambulizi ya wavamizi wa kizayuni.

- Shule na vyuo vikuu 136 vimeharibiwa kabisa na wavamizi.

- Shule na vyuo vikuu 335 vimeharibiwa mfululizo.

- Wanafunzi 12,794 waliuawa katika vita.

- Wanafunzi 785,000 wamenyimwa elimu wakati wa vita.

- Walimu na wafanyakazi 756 wa sekta ya elimu wameuawa Shahidi.

- Maprofesa na watafiti 149 wa vyuo vikuu wameuawa.

- Misikiti 823 imeharibiwa kabisa.

- Misikiti 158 imeharibiwa kwa kiasi.

- Makanisa 3 yameharibiwa.

- Makaburi 19 kati ya jumla ya 60 yameharibiwa kabisa na kwa kiasi.

- Miili 23,000 imeibiwa kutoka kwenye makaburi na wavamizi wa kizayuni.

- Makazi 161,600 yameharibiwa kabisa.

- Makazi 82,000 hayafai kwa kuishi ndani yake.

- Makazi 194,000 yameharibiwa kwa kiasi.

- Tani 88,000 za vilipuzi zimedondoshwa kwenye Ukanda wa Gaza.

- Hospitali 34 ziko nje ya mzunguko wa utoaji wa huduma.

- Vituo vya matibabu 80 viko nje ya mzunguko wa utoaji wa huduma.

- Taasisi za matibabu 162 zimelengwa (kwa kushambuliwa).

- Magari 136 ya kubebea wagonjwa yalishambuliwa na wavamizi wa kizayuni.

- Athari 206 za kihistoria zimeharibiwa.

- Kilomita 3,130 za mtandao wa usambazaji umeme zimeharibiwa.

- Transfoma 125 za ardhini zimeharibiwa.

- Mita 330,000 za mtandao wa usambazaji wa maji zimeharibiwa.

- Mita 655,000 za mtandao wa maji taka zimeharibiwa.

- Mita 2835,000 za mtandao wa barabara na mitaa zimeharibiwa.

- Majengo 42 na kumbi za michezo zimelengwa na kuharibiwa.

- Visima 717 vya maji vimeharibiwa na havitumiki.

- 88% ya Gaza imeharibiwa kabisa.

- Dola bilioni 37 ni makadirio ya uharibifu wa awali wa moja kwa moja wa mauaji haya makubwa ya kimbari dhidi ya Gaza.