Main Title

source : Abna
Alhamisi

9 Januari 2025

20:26:52
1521635

Kwa uwepo wa Ayatollah Ramadhani; Mkutano wa ndani wa Ahlul-Bayt (a.s) wa Bangladesh ulianza kufanya kazi

Kwa uwepo wa Ayatollah Ramezani, Mkutano wa ndani wa Ahl al-Bayt (a.s) wa Bangladesh ukihudhuriwa na sehemu tofauti za Mashia wa nchi hii umeanza kazi yake katika hafla.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (a.s) - ABNA - Baraza la ndani la Ahlul Bayt (a.s) la Bangladesh lilianzisha hafla iliyohudhuriwa na na makundi mbalimbali ya Shia wa nchi hiyo na kufanya chaguzi za kupiga kura za Wajumbe wa Bodi ya Mkutano.

Ayatollah Reza Ramezani, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s), ambaye alikuwepo kama mgeni katika hafla hii, aliashiria juu ya umuhimu wa kupanga (mipango) na kusema: Makundi yote yanapaswa kufikiria juu ya mpangilio. Leo, vyama vya wafanyakazi vimefafanuliwa duniani na kila chama cha wafanyakazi kinaundwa ili kutekeleza kazi yao. Imam Musa Sadr alisema huko Qom miaka 60 iliyopita kwamba Ukristo una nafasi ya kwanza katika Mashirika ya Kidini Duniani.

Katika eneo la Kusini mwa Lebanoni, kuna familia moja au mbili za Kikristo, na kwao msomi Mkristo anatumwa Jumapili ili kuendesha ibada.

Pia, kwa mujibu wa Imam Musa Sadr, Chuo Kikuu cha Al-Azhar cha Misri na Seminari (Hawzat) za Kisunni zina nguvu katika suala la mpangilio, lakini Mashia ni dhaifu katika uwanja wa kazi ya kiushirika (na kimpangilio).

Aliendelea: Katika utamaduni wa Kishia, ni muhimu kuanzisha ushirika katika miji na nchi nzima. Mashia wote katika mji wanapaswa kuwasiliana wao kwa wao, na katika nchi, kuwe na mawasiliano kati ya wawakilishi wa Mashia katika miji tofauti tofauti; hii inaunda nguvu na kuimarisha ushirikiano wa makundi yote.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) amesema kuhusu Jumuiya ya Ahlul-Bayt (a.s) huko Bangladesh:

Mkutano huu unatoa fursa kwa Misikiti yote, Hussainiyyah zote na vituo vyote vya Mashia vya nchi hii kukusanyika pamoja na kuchukua hatua za pamoja za kukuza mafundisho ya Shule ya Ahlul-Bayt (a.s). Mkutano wa Ahl al-Bayt (a.s) wa Bangladesh unawaalika watu kwa Mwenyezi Mungu na Ahlul-Bayt (a.s), na kama Ahlul-Bayt (a.s) ndio kiini na mhimili (wetu unaotuunganisha), basi hatutakuwa na sababu ya kutokukubaliana.

Ameongeza kuwa: Bunge la Ahl al-Bayt (a.s) la Bangladesh linaweza kuwa na sehemu tofauti, wakiwemo vijana; Sehemu ya Jumuiya ya vijana inapaswa kuandaa kambi za mafunzo kwa vijana katika miji tofauti ya Bangladesh na kuwafundisha masomo mbalimbali katika kambi hizi.

 Pia inawezekana kuanzisha chama cha wanawake au kikundi cha kazi cha wanawake chini ya Bunge la Ahl al-Bayt (AS) la Bangladesh. Kwa sababu kuna wanawake wengi wanaofanya kazi katika miji tofauti ya Bangladesh.

Ayatollah Ramezani aliendelea kusema: “Wamagharibi wanadai kuwa tunainua hadhi ya Wanawake, na badala ya kuwainua wameshusha hadhi yao, lakini Dini inashikilia msimamo wa Hadhi ya Mwanamke, na Uislamu ndio Dini inayotetea zaidi katika uwanja wa kudumisha Hadhi na Haki za Wanawake".

Wamagharibi waliruhusu ukatili mbaya zaidi dhidi ya Wanawake na kutokana na ukatili huu, ufeministi ulizaliwa (na kuwepo).

Katika hitimisho, alisema: Wale wanaodai Haki za Binadamu wanapaswa kusoma masomo ya Imam Sajjad (a.s) ili kuelewa Haki za Binadamu ni nini. Na ndio maana, tunaona kuna maandiko mengi yenye nguvu zaidi ya utetezi wa Haki za Binadamu katika Qur'an Tukufu na katika maneno ya Ahlul-Bayt (a.s).