Main Title

source : khabarfarsi
Ijumaa

5 Juni 2015

20:41:17
693906

Makombura ya zilzala yajeshi la Yemen yalipua sehemu ya Dhaharini nchini Saudi Arabia

Jeshi la wananchi naserikali ya Yemen wakijibu mashambulizi ya uvamizi wa Saudi Arabia kwakuendeleza kufanya mashambulizi kwa makombora ya Zilzala katika makambi ya jeshi la Saudi Arabia na baadhi ya mikoa iliopo katika mipaka ya nchi hiyo na Saudi Arabia

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kutoka shirika la khabarifarsi: majeshi ya Yemen yameanza kujibu mashambulizi hayo kwa wavamizi wa taifa la Yemen kwakupiga makombora ya aina ya Zilzala yanayozalishwa ndani ya nchi hiyo katika makambi ya majeshi ya Saudia.
Majeshi ya Yemen lengo ya kufanya mashambulizi hayo na kutumia silaha hizo ni kusambaratisha kambi za kijeshi ya ya utawala Saudi Arabia katika sehemu ya Dhahrani kusini mwa mkoa wa Asir na kusababisha maafa ya vifaa vya kijeshi nakujeruhi wanajeshi kadhaa, ama Kambi iliopatwa na maafa zaidi ni kambi ya kijeshi ya Al-Hamamah iliokaribu na Boda ya Alab.
Vilevile jeshi la Yemen limeangamiza magari ya kijeshi yaliokuwa katika boda ya Alab na kusababisha hasara kubwa kwa jeshi hilo la Saudi Arabia.
Majeshi ya Yemen bado yanaendelea kufanya mapambanao yake kwaajili ya kuikomboa bandari ya Almansura kutoka mikononi mwa vikundi vya kigaidi vya Alqaida katika mkoa wa Adni kusini mwa Yemen.
Kwamujibu wa ripoti hii kamati ya jeshi la mapinduzi ya Yemen linalenga kukata mawasiliano ya kimtandao katika kambi ya kijeshi ya Almzahaf iliopo sehemu ya jiyzan nchini Saudi Arabia.