Main Title

source : Pars Today
Jumatatu

10 Juni 2019

06:43:03
948971

Ukwamishaji mambo wa Juan Guaidó kuhusu mgogoro wa kisiasa wa Venezuela

Kuendelea mgogoro wa kisiasa nchini Venezuela na kadhalika kushindwa wapinzani wa nchi hiyo kumng'oa madarakani Rais Nicolás Maduro, kumepelekea Juan Guaidó, kiongozi wa upinzani kukubali pendekezo la upatanishi wa Norway na kuanza mazungumzo ya wawakilishi wa serikali na wapinzani huko mjini Oslo.

(ABNA24.com) Kuendelea mgogoro wa kisiasa nchini Venezuela na kadhalika kushindwa wapinzani wa nchi hiyo kumng'oa madarakani Rais Nicolás Maduro, kumepelekea Juan Guaidó, kiongozi wa upinzani kukubali pendekezo la upatanishi wa Norway na kuanza mazungumzo ya wawakilishi wa serikali na wapinzani huko mjini Oslo.

Pamoja na hayo, katika hatua yake mpya ya ukwamishaji mambo katika juhudi za kutatua mgogoro wa kisiasa wa Venezuela, Guaidó amedai kwamba wapinzani walio chini yake hawana nia ya kushiriki duru mpya ya mazungumzo nchini Norway yatakayohudhuriwa na wawakilishi wa serikali. Kadhalika kiongozi huyo wa upinzani amesema: "Hivi sasa sio wakati wa mazungumzo zaidi, kwa nini? Kwa kuwa mambo hayaendi vizuri na Maduro hajajiuzulu, hivyo mazungumzo hayana faina yoyote." Duru ya zamani ya mazungumzo ambayo ilifanyika Oslo, mji mkuu wa Norway hapo mwezi Mei mwaka huu, ilivunjika pia kutokana na Juan Guaidó kuendelea kusisitizia suala la Rais Nicolás Maduro kuondoka madarakani. Chama tawala cha Kisoshalisti kiliomba upatanishai wa Noryaw kwa ajili ya kutatuliwa mgogoro wa nchi hiyo ya Amerika ya Latini, hata hivyo wapinzani hawakuwa tayari kushiriki mazungumzo hayo huku wakidai kwamba Rais Maduro anatumia anga hiyo kwa ajili ya kuendelea kusalia madarakani. Aidha tarehe 25 Mei mwaka huu Guaidó sambamba na kuyataja kuwa yasiyo na thamani mazungumzo na serikali ya Caracas nchini Norway, alitangaza kwamba ataendeleza wimbi la maandamano ya kuishinikiza serikali ya nchi hiyo iweze kujiuzulu.

Alisisitiza kwamba wapinzani wamejibu tu pendekezo la serikali ya Oslo kwa ajili ya upatanishi na si vinginevyo. Kwa mtazamo wa Guaidó njia yoyote ya utatuzi wa mzozo wa Venezuela lazima ijumuishe kujiuzulu Rais Nicolás Maduro na kisha serikali ya mpito kutoa ruhusa ya kufanyika uchaguzi wa rais. Ukweli ni kwamba kwa mtazamo wa kiongozi huyo wa upinzani, mazungumzo hayo yanapasa kuwa na natija moja tu nayo ni ya kuondoka madarakani Rais Maduro na kufanyika uchaguzi mpya wa rais. Katika uwanja huo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani pia sambamba na kuunga mkono msimamo wa Juan Guaidó imesema: "Tunataraji kwamba mazungumzo ya mjini Oslo yatajikita juu ya suala hilo, (kuondoka madarakani Rais Maduro) na hapo ndipo kutakaposhuhudiwa maendeleo katika mazungumzo hayo." Hatimaye tarehe 29 Mei mwaka huu, wapinzani wa Venezuela walitangaza kupinga pendekezo la kuendelea na mazungumzo kwa ajili ya kufikiwa njia ya utatuzi wa kisiasa wa mzozo wa nchi hiyo. Aidha tarehe 23 Januari mwaka huu kupitia uungaji mkono kamili wa Marekani, Guaidó alitilia shaka uhalali wa kisheria wa Rais Maduro nchini Venezuela, hatua ambayo iliamsha moto wa mgogoro wa kisiasa nchini humo.

Mkabala wake, Rais Maduro alimtaja Guaidó kama mwanasesere wa Marekani kwa ajili ya kudhamini malengo ya Washington nchini humo. Katika miezi ya hivi karibuni Marekani katika uungaji mkono wake kwa Guaidó imezidisha mashinikizo ya kisiasa na kiuchumi kwa Rais Maduro kwa lengo la kumlazimisha ajiuzulu. Pamoja na hayo juhudi hizo za Washington zimeendelea kufeli. Wakati huo huo Washington imeshadidisha mashinikizo ya kila upande dhidi ya Venezuela kukiwemo kuiwekea vikwazo tofauti serikali ya Caracas na hata kutishia kuishambulia kijeshi kwa maslahi ya wapinzani. Wakati huo huo upinzani wa kimataifa unaoitaka serikali ya Trump kukomesha uingiliaji wake katika masuala ya ndani ya Venezuela hususan wa nchi za Russia, China na Iran, nao umeendelea kuongezeka. Katika uwanja huo serikkali ya Russia kama mmoja wa washirika wakubwa wa serikali ya mrengo wa kushoto ya Venezuela, sambamba na kumuunga mkono Rais Maduro imetoa onyo kali kwa uingiliaji wowote wa kijeshi wa Marekani katika nchi hiyo ya Amerika ya Latini. Tarehe sita ya mwezi huu Rais Vladmir Putin wa Russia aliutaja uingiliaji wowote wa kijeshi wa Marekani nchini Venezuela kama janga kubwa na kusisitiza: "Sisi tutaendeleza ushirikiano wetu na Venezuela. Tupo ndani ya nchi hiyo na tutaendelea kuwepo."





/129