Main Title

source : Pars Today
Jumatatu

15 Julai 2019

05:55:47
961150

Kuendelea hatua ya Uingereza ya kuuzia silaha utawala wa Aal Saud

Serikali ya Wahafidhina nchini Uingereza imekuwa na nafasi kubwa katika vita vya Yemen kwa kuendelea kuuzia silaha muungano vamizi unaoongozwa na Saudia.

(ABNA24.com) Licha ya kuwepo malalamiko makubwa nchini Uingereza ukiwemo pia upinzani wa mahakama ya rufaa ya nchi hiyo, lakini bado London imekusudia kuendeleza mwenendo wake huo. Katika uwanja huo, mtandao wa gazeti la The Independent umeandika kuwa, serikali ya Wahafidhina nchini Uingereza licha ya uamuzi wa mahkama ya rufaa wa kupinga suala hilo, lakini bado serikali hiyo imekusudia kuendelea kuiuzia Saudia silaha. Mawaziri wa serikali ya Uingereza wanalalamika na kuichukulia marufuku ya kuiuzia silaha nchi hiyo ya Kiarabu iliyotolewa na mahkama hiyo kuwa isiyo ya kisheria. Siku chache zilizopita mahkama ya rufaa ya Uingereza ilitoa hukumu na kubainisha kwamba serikali ya Wahafidhina ya nchi hiyo imekiuka sheria inayohusiana na mauzo ya silaha sambamba kwa kuruhusu silaha hizo ziuziwe utawala wa Saudia, silaha ambazo yumkini zikawa zinatumika katika vita nchini Yemen.

Katika uwanja huo Terence Etherton, jaji wa mahkama hiyo akitoa hukumu aliitaka serikali ya London kusitisha mara moja mauzo ya silaha kwa serikali ya Riyadh. Katika kikao kilichofanyika miaka miwili iliyopita mahkama ya nchi hiyo ilitoa hukumu ya kuendelea mauzo ya silaha kwa Saudia bila kizuizi, hata hivyo kampeni inayopinga biashara ya mauzo ya silaha ya 'CAAT' sambamba na kuwasilisha ushahidi mpya unaoonyesha ukubwa wa jinai zinazotekelezwa na utawala wa Aal-Saud nchini Yemen na kadhalika kiwango cha uharibifu wa vita hivyo, ilipelekea faili hilo kutumwa katika mahkama ya juu iliyotaka kukomeshwa haraka ushirikiano wa silaha kati ya nchi mbili hizo. Kampeni ya kupinga biashara ya silaha imesema kuwa biashara ya mauzo ya silaha kwa Saudia, inakinzana na sheria na kuwa  ndege za kivita na mabomu yaliyotengenezwa Uingereza yamekuwa yakitumika katika kuwaua raia wa Yemen. Andrew Smith, msemaji wa kampeni hiyo amesema kuwa: "Si jambo la kushangaza kuona serikali inafanya juhudi kubwa za kulinda mauzo yake ya silaha kwa Saudia." Mbali na mashirika ya haki za binadamu na asasi za kupinga mauzo ya silaha, chama cha upinzani cha Leba pia kimekuwa kikatangaza upinzani wake kuhusiana na mwenendo wa sasa wa serikali ya London wa kuiuzia silaha Saudia na kimetaka kukomeshwa suala hilo mara moja.

Katika uwanja huo, Jeremy Corbyn, Kiongozi wa Chama cha Leba nchini Uingereza na katika msimamo wake mpya amekosoa kitendo cha serikali cha kutofungamana na ahadi zake juu ya kukoma kuwauzia silaha Wasaudi na kuongeza kuwa, London hailipi umuhimu wowote suala la maisha ya raia wa Yemen. Corbyn amesema: "Hatua hiyo ya mawaziri wa serikali (ya Uingereza) ni yenye kufanyia maskhara ahadi yao ya kukomesha mauzo ya silaha, tena katika hali ambayo kunafanyika uchunguzi wa maafa ya raia nchini Yemen. Kipaumbele cha serikali ya (Wahafidhina) ni mauzo ya silaha na si kulinda haki na roho za wananchi wa Yemen." Licha ya ripoti mbalimbali za asasi na mashirika ya haki za binaadamu kuhusiana na mauaji dhidi ya raia wa Yemen, kushambuliwa maeneo na asasi za kiraia za nchi hiyo kunakofanywa na ndege za Saudia na washirika wake na kulaaniwa kila mara utawala wa Aal Saud kutokana na ukiukaji wake wa haki za binaadamu hususan baada ya kutekeleza mauaji dhidi ya Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari na mkosoaji maarufu wa utawala wa Riyadh, lakini bado Uingereza kwa kushirikiana na Marekani zinaendelea kushirikiana na Saudia katika vita vyake vya kichokozi nchini Yemen. Kuhusiana na suala hilo, Barbara Valey, mtaalamu wa masuala ya kisiasa anasema: "Marekani na Uingereza ni wahusika wa vita vya maafa makubwa na jinai za kivita nchini Yemen." Hii ni kusema kuwa tangu vilipoanza vita vya Yemen mwezi Machi 2015, serikali ya Uingereza ilitoa kibali cha mauzo ya silaha zinazokaribia pauni bilioni tano kwa Saudia kama ambavyo pia imekuwa na nafasi chanya katika kutoa mafunzo kwa askari wa Saudia.



/129