Afya ya jamii

Dawa bandia za Malaria zaongeza madhara

  • Habari NO : 291321
  • Rejea : ABNA
Ikilezwa kuwa katika miaka 2009-2011 Dawa bandia zimekuwa zikizidi katika Nchi za Afrika Lengo kuendelza ugonjwa huo na kuonyesha kuwa bara la Afrika ni masikini na.. wataalamu wa maswala ya afya katika bara la Afrika wanapaswa kuchukua hatua kambambe za kusitisha kuenea kwa dawa hizo bandia katika bara la Afrika au sio mamilioni ya watu watafariki.

Ripoti ya ABNA- Wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza wamesema kuwa ongezeko la dawa bandia barani Afrika, ni pigo kubwa katika juhudi zinazoendelea za kupambana na maradhi ya Malaria.

Malaria huwaua karibu watu milioni moja kila mwaka katika bara la Afrika.

Wanasayansi wa chuo hicho wamesema kuwa kuuzwa kwa dawa hizo bandia huwadhuru wagonjwa mbali mbali na kusababisha wagonjwa hao kutoweza kupata tiba kamilifu wanapotumia dawa sahihi.

Wataalamu hao wa dawa walisema baadhi ya dawa hizo bandia zinatoka Uchina

Wameshauri kuwa wataalamu wa maswala ya afya katika bara la Afrika wanapaswa kuchukua hatua kambambe za kusitisha kuenea kwa dawa hizo bandia katika bara la Afrika au sio mamilioni ya watu watafariki.

Watu walio taabani sana kutokana na dawa hizo bandia ni watoto na wanawake waja wazito.


پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni