Mafunzo ya Jamii

Ukhalifa wa Omar na kuungwa mkono.

  • Habari NO : 291535
  • Rejea : ABNA

Abubakar aliposhikwa na maradhi alimwita Athman na akamwambia: Andika kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu, haya ni aliyoamua Abubakar bin Quhafah kwa Waislamu, Amabaad. Abubakar akazimia, Athman akaandika, ama baad, mimi ni memfanya Omar bin Al-Khatab kuwa Khalifa wenu na sikuwatawalisheni mtu mwema kisha Abubakar akazinduka, akasema: Na kuona uliogopa watu kukhitalifiana kama ningekufa katika kuzimia kwangu, akasema: Ndio, akasema Mungu akulipe kheri kwa ajili ya Uislamu na watu wake. Abubakar akaafiki haya.

Kama ilivyopokelewa kwamba Omar alikuwa na karatasi ambayo humo Abubakar alimteua kuwa Khalifa na alikuwa anawaambia watu sikilizeni na tiini kauli ya Khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, anasema kwamba: Hakika mimi sikuwatawalisheni mtu mwema.

Na inabainika kwamba Abubakar alikuwa anaogopa ikhitilafu kwa watu baada yake na kugombania Ukhalifa kwa watu baada yake na kugombania Ukhalifa hivyo akamuusia Omar na akaandika katika karatasi ili iwe ni hoja kwa watu, na ili kusiwepo na nafasi ya kugombania.

Swali ambalo linajitokeza hapa ni Mtume (s.a.w.w.) hakufikiria kama alivyofikiria Abubakar? Au hakuogopa ikhitilafu na ugomvi katika umma juu ya uongozi kama alivyoogopa Abubakar?

Na tofauti ilikuwa kiasi gani baina ya hali ya waislamu wakati alipofariki Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na hali yao wakati wa kufariki Abubakar? Je, dhana ya kukhitalafiana na kufarakana baada ya kufariki kwake (S.AW.W) ilikuwa ni kubwa zaidi na hiyo ni kwa sababu tulizozitaja mwanzo, hatari ya kuritadi Wanafiki, Warumi waliokuwa wanasubiri kuwabadilisha Waislamu wakati watakapo pata fursa, tukiachilia mbali ugomvi wa kikabila baina ya Mabedui? Au Mtume (s.a.w.w.) hakufahamu hatari zote hizi zinazosubiri Uislamu na watu wake kama alivyo fahamu Abubakar?

Hakika ni ajabu ya maajabu, pamoja na hadithi zote zilizothibiti za Mtume (s.a.w.w.) kumfanya Ali (as) kuwa Khalifa - kama ilivyo tangulia - wote walipinga kwa hoja ya kuwa Mtume (s.a.w.w.) alifanya jambo la Ukhalifa liwe Shura baina ya Waislamu - rejea matukio ya Saqifa utaona ni aina gani ya Shura ilitumiwa bayia ya Abubakar- na Abubakar anamfanya Omar kuwa Khalifa wa Waislamu kwa kauli yake bila ya kumshauri yeyote katika Waislamu, iko wapi Shura wanayoidai? Bila shaka watasingizia msimamo huu kuwa Abubakar ana haki ya kumteua yeyote amtakaye kati ya Waislamu anayeona kuwa anafaa kubeba jukumu la Ukhalifa pamoja na kwamba alikuwa naumwa sana wakati wa kuchukua uamuzi huo ambapo alizimia wakati wa kuandika kwake, halafu Athman akakamilisha badaa yake. Athman ambaye alikuwa anajua kuaminiana kati ya Makhalifa wawili, kwa Sababu Omar bin Al-Khatab alisimama msimamo mkali ulioshuhudiwa siku ya Saqifa katika kumsaidia Abubakar kupata Ukhalifa. La ajabu na lakushangaza ni kwamba hakusema yeyote kati ya Masahaba kuwa Abubakar alikuwa anaweweseka wakati alipoandika wasia kama ambavyo walimwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) neno hilo wakati alipowaamuru wamletee karatasi awaandikie ili wasipotee baada yake na wakamkataza kuandika wasia wake katika karatasi ambapo ilikuwa inawezekana kumpa Ukhalifa Imam Ali (A.S) na kuwaonyesha ushahidi kama alivyoonyesha Omar karatasi hiyo ambayo Abubakar alimwandikia kuwa Khalifa.


پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni