UTAFANYA NINI ILI UFAANIKISHE NDOA YAKO?!

  • Habari NO : 322381
  • Rejea : Hasanul Mujtaba

Vitabu na Makala nyingi zimeandikwa kuelezea masuala ya kifamilia na kufafanua umuhimu na maana ya familia, katika kila nyanja inayohusu familia.

Uandishi wa Vitabu na Makala hizo haukuweza kuathiri jamii ipasavyo kwani kadiri siku zinayokwenda ndivyo Jamii inaporomoka na kupoteza Tamaduni zake, na sababu ya kutoathiri Vitabu na Makala hizo ni kuwa kwake kinyume na mafunzo ya Mtukufu Mtume Muhammad(s.a.w.w) .

Katika Makala hii tutajitahidi kuelezea nini la kufanya ili tufanikishe ndoa zetu, na kuzifanya ndoa hizo ziwe ni zenye mafanikio katika jamii.

Katika kujenga Familia kuna mambo kadhaa ni vyema kuzingatiwa kabla ya kuanza maisha ya ndoa ;

1-Kufahamu ukoo na nasaba ya pande zote mbili(upande wa Kiume na Wakike).

Suala hili ni muhimu sana kwa watu wanaotaka kuishi pamoja kwani ndio lenyekuonyesha mustakabali wa wanandoa na familia, ambapo wazee wetu wa kale walikisisitiza kuhusu suala hilo.

2-Kuchunga hali ya kiuchumi kwa pande zote mbili, tajiriba inaonyesha kuwa famila zinazo pishana kiuchumi kwakiwango kikubwa, mara nyigi hazifanikiwi hivyo mnapaswa kuzingatia suala hilo.

 3- Kiwango cha Elimu kwa pande zote mbili,hususan mwanamke hatakiwi kuwajuu kielimu zaidi ya mwanaume.

 4-Umri wa wanandoa watakiwa usipishane kwa asilimia kubwa.

 Masuala haya na mengineyo mengi yaweza kuwa ni sababu ya mafaanikio kama yatazingatiwa, au kinyume chake endapo yatapuuzwa.

Pia tukitaka familia zetu ziwe bora ni lazima kuzingatia mambo haya baada ya kutekeleza  mambo kadhaa yaliyotajwa hapo awali, nayo ni yafuatayo:

Nyumba ya wanandoa  ni lazima ishamiri Upendo, Utulivu na Huruma baina yao, mambo haya matatu ndio chanzo na msingi mkubwa wa kufanikisha maisha ya Ndoa na kinyume na hayo Ndoa itapoteza maana yake asili, kwani ni jambo lisilo wezekana kwa yoyote anaetaka kujenga mahusiano ya ndoa kufanikisha suala hilo pasina kuwepo upendo baina yao isipokuwa yale mahusiano yasio ya kisheria.

Katika kusisitiza suala hilo Mwenyezi Mungu mtukufu anasema katika Qur`an tukufu:

وَمِنْ آَيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُمْ مِنْ أَنْفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُمْ مَوَدَّةً وَرَحْمَةً إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآَيَاتٍ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ

 “Na katika aya zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao, na ameweka mapenzi na huruma baina yenu, hakika katika haya bila shaka ni Ishara kwa watu wenye kutafakari.” Surat Ar-Rum 21

Suali la muhimu ni kwamba; Maneno ya Mwenyezi Mungu ya ashiria kuwa ndoa ni upendo , kwa mantiki hii kwanini mwa sisitiza upendo katika ndoa ilhali ya kuwa yenyewe ni upendo?!!

Ni kweli ndoa ni upendo ila upendo huu ni kama shamba, lahitaji miundo mbinu ili kupata matunda mema, na miungoni mwa miundo hiyo ni kufahamu kwanza Ardhi kuwa inauwezo gani wakuzalisha mazao na ni mazao gani yanayofaa katika Ardhi hiyo na zaidi hukaguliwa kabla ya kilimo.

Upendo katika ndoa ndio nguzo muhimu na kwa kuzingatia hilo utakuwa umeandaa mafaanikio ya  ndoa na familia yako, ndoa ni Shamba lilomwagiliwa maji na kutoa matunda mema, na matunda ya ndoa ni utulivu na uaminifu baina ya pande mbili ili kuandaa mazingira mazuri kwa kizazi kijacho.

Ili kuepuka kurefusha makala hii hakuna budi kueleza njia rahisi ya ufanikishaji wa ndoa na kuendeleza mapenzi na upendo ndani ya familia, ili kufaanikisha hilo lazima ufate njia zifuatazo;

1-Zidisha kusema kauli hii(NAKUPENDA) katika nyumba yako, na kumwambia  kila mmoja katika familia yako hata Mtoto mchanga.

Imepokelewa kutoka kwa Mtukufu Mtume Muhammad(s.a.w.w) anasema katika kuashiria hilo:

قول الرجل للمرأة إني أحبك لا يذهب من قلبها أبداً.

“Kauli ya Mwanaume(Mme) kumwabia Mwanamke(Mke), hakika mimi nakupenda,  kamwe (neno hili)hailtatoka moyoni mwake milele”

Imam Jaafar Sadiq(as) nae anasema:        

إن الله ليرحم الرجل لشدة حبه لولده

“Hakika Mwenyezi Mungu humsamehe Mja kwa kushdidisha mapenzi kwa mwanawe.”

2-Zidisha kubusu watu wa familia yako, Watoto na...

”imepokelewa kuwa siku moja alikuja mtu kwa Mtume(saw) na akamwambia Mtume(saw): Kamwe sijawahi kumbusu Mtoto, na alipoondoka Mtu yule Mtume(saw) aliwambia watu akisema: Mtu huyu niliekuwa nae ni wa motoni”

Ndugu msomaji mambo haya ni madogo kiasi huonekana hayanafaida yoyote kwa watu wa kawaida ila athari yake ni kubwa.pia ukizingatia mambo hayo bila shaka utafanikiwa katika ndoa na maisha ya familia yako.


پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni