MAFUNZO YA SWALA

  • Habari NO : 400550

أَقِمِ الصَّلاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلى‏ غَسَقِ اللَّيْلِ وَ قُرْآنَ الْفَجْرِ إِنَّ قُرْآنَ الْفَجْرِ كانَ مَشْهُوداً 

(Simamisha Sala jua linapo pinduka mpaka giza la usiku, na Qur'ani ya al fajiri. Hakika Qur'ani ya alfajiri inashuhudiwa daima.) QURAN 17/87

MAFUNZO YA SWALA SAHIHI

Kwanza kabisa,lazima mwenye kuswali ahakikishe ametoa Adhana kisha Iqama(yaani:Kukimu kwa ajili ya kusimamisha swala).

Baada ya ADHANA na IQAMA basi hapo inafuatia TAKBIRATUL-IHRAM (الله أکبر).

Swala inaanza kwa kutamka Takbir hii, ukisha itamka basi hapo tayari swala imeanza na inaisha kwa kutoa salam.

Baada ya utangulizi huu mfupi, sasa ni wakati wa kuyatizama yale mambo ambayo ni wajibu katika swala.

MAMBO YA WAJIBU KATIKA SWALA

Mamabo yawajibu katika swala ni kumi na moja (11).Lazima mwenye kuswali ahakikishe mambo hayo kumi na moja ameyatenda kama inavyotakiwa.Katika mambo haya kumi na moja (11) ya wajibu kuna matano (5) ni RUKNI (Yaani:Ni nguzo za Swala) na mengine sita(6) yaliyobaki si RUKNI katika swala.Na inaposemwa “RUKNI ZA SWALA”,humaanishwa NGUZO ZA SWALA,kwa maana kwamba:Swala imesimama katika nguzo hizo tano,ikitokea nguzo moja ikaharibika au isitendeke kama inavyotakiwa au ikasahaulika katika swala basi swala itakuwa si sahihi,mwenye kuswali atatakiwa kurudia swala yake,ama yale mambo sita(6) ambayo sio nguzo za swala,ikitokea moja wapo kati ya hayo (sita) ikasahaulika ktk swala au kutendeka isivyotakiwa basi swala haitaharibika au tuseme:Haitakuwa batili,bali itakuwa ni swala sahihi,maana kukosea au kusahau katika hayo mambo sita ambayo si nguzo ktk swala hakuharibu swala wala kuibatilisha,ispokuwa makosa hayo au kusahau huko kukitokea ktk moja wapo ya nguzo za swala ambazo tutazitaja hivi punde.

MAMBO YA WAJIBU KTK SWALA NA AMBAYO NI RUKNI ZA SWALA/ NGUZO ZA SWALA

Nguzo za swala ni tano:

1- NIA

Nia si lazima utamke kwa maneno kwamba,nina swali swala ya dhuhri yenye rakaa nne,kurbatan ila llah,si lazima uimbe nia namna hiyo bali nia inatosha kile ulichokiazimia moyoni mwako,maana ile kuchukua maji,ukatia udhu,tayari ushajenga nia ktk moyo wako na ktk akili yako kwamba sasa naelekea kwenye swala fulani.Nia maana yake ile azma yako kunako unachotaka kukitenda,si sharti uanze kuitaja kwa maneno.Mfano;Msafiri anaetaka kuelekea sehemu fulani,huwa anatia nia kuwa kesho au sasa hivi ninasafiri kuelekea sehemu fulani,nia hiyo huwa ipo moyoni,na ile kutoka kuelekea kituo cha basi hutosha kabisa kudhihirisha nia yake ya safari yake.

Hivyo nia hutimia pasina kutamkwa na ile kutakwa sio sharti ktk Nia,bali unaweza kuitamnka tu kwa ulimi na isitimie,maana kutimia kwa nia ni pale inapohudhuria moyoni kiasi kwamba akili ya mwenye kuswali inakuwa haiwazi kitu kingine tofauti na swala na kwamba sasa yupo mbele ya Mwenyeezi Muingu (s.w).Hiyo ndiyo nia ambayo unatakiwa kuileta mwanzo wa swala na iendelee kuwepo hadi mwisho wa swala.Hivyo nia sio mwanzo wa swala tu bali iwepo hadi mwisho kabisa wa swala yako.

2- QIYA’M (Kusimama wima).

3-  TAKBIRATUL-IHRAM(Takbir ya kuhirimia swala na ambayo inaashiria mwanzo wa swala kwamba sasa swala imeanza). 

4- RUKUU (Kurukuu).

5 - SUJUD (Kusujudu).

MAMBO YA WAJIBU KTK SWALA NA AMBAYO SIO RUKNI ZA SWALA/ SIO NGUZO ZA SWALA

6- Qira’a :(Kusoma Suratul Fatiha,yaani:Al-Hamdu,kisha Sura yoyote).

Sura unayoisoma lazima uisome kuanzia mwanzo hadi mwisho,hairuhusiwi kusoma sura nusu,rakaa ya kwanza kisha kusoma nusu iliyobaki katika rakaa ya pili.Bali inatakiwa isomwe sura kamili mwanzo hadi mwisho.Mfano huruhusiwi kusoma KULI HUWALLAH AHAD NUSU YAKE NA KUMALIZIA NUSU ILIYOBAKI KATIKA RAKAA YA PILI,NA HIVYO HIVYO KTK SURA YOYOTE ILE UTAKAYOISOMA KTK SWALA.

Hapa lazma tuweke wazi:Ukichunguza swala za walio wengi ktk madh-hebu ya Ahlus-sunna,utakuta baada ya kusoma Al-hamdu,basi mtu anasoma sura yoyote ndefu kama Suratul-Baqarah kama Aya kumi kisha anarukuu,kisha anarudi rakaa ya pili anasoma Aya zingine kama ishirini au kumi na tano au zozote atakazoweza kutoka sura nyingine kama vile Suratun-Nisaa kisha anaurukuu!.Lakini kwa mujibu wa mafunzo sahihi tunayofundishwa au iliyofundishwa na Maimam wetu watukufu (a.s) kutoka Nyumba ya Mtume (s.a.w.w) ambao hakuna shaka yoyote (wala chembe ya shaka kwamba) wanaijua vizuri zaidi swala ya Mtume (s.a.w.w),swala sahihi lazima ktk QIRAA isomwe sura kamili ana sio nusu sura au robo yake au nusu robo.Na hivyo ni bora mwenye kuswali au kuswali kama Imam asome sura fupi ktk swala ambazo atakuwa na uwezo wa kuzisoma mwanzo hadi mwisho na sio kusoma sura ndeeefu wakati anajua anawaongoza watu ambao wanatofautiana hali zao za kiafya.Hivyo zisomwe sura kamili na sio nusu sura,ktk qur’an sura fupi zimo nyingi sana unazoweza kuzisoma kwa ukamilifu kama vile Suratun-naziat,surat Abas,surat-tak-wiyr,suratul-infi-twaar,suratul-mutwaffifiin,suratul-inshiqaaq,suratul-buruuji,Suratu-twaariq,suratul-a’ala,suratul ghashiya,suratul-fajri,suratul-balad,suratul-lail,suratul-qadr,suratul-bayyina,suratul-kaafirun,suratun-nasri,suratul-ikhlaaswi,suratul-falaq,suratun-naasi,na zingine nyingi tu.

7-Dhikr

8-Tashahhud

9-Salam

10-Tartib: (Kwa maana kwamba:Swala lazimwa iswaliwe kwa kufuata utaratibu huu,kuanzia Takbiratul-Ihram,kisha hatua Qira’a,kisha Rukuu,kisha sujud,kisha ukae ktk rakaa ya pili baada ya sajda usome TASHAHUD,ukimaliza ndio usimame kwa kwa ajili ya rakaa ya tatu,kisha ukae ktk rakaa ya mwisho usome TASHAHUD,na baada ya Tashahud umalizie kwa Salam,swala inatakiwa iwe ktk utaratibu huo au tuseme ifuate utaratibu huo,sio unaanza na Takbiratul-Ihram,kisha unaingia sajda,unaacha qira’a na rukuu,namna mwenye kuswali atakuwa hajafuata utaratibu,na atahesabika anaswali anavyotaka na sio inavyotakiwa).

11-Muwalaat: Yaani: Lazima mwenye kuswali ahakikishe anaswali swala yake kwa kufuatanisha vitendo pasina kuacha gape au nafasi bain aya kitendo na kitendo.Mfano:Baada ya Takbiratul-ihram,unaingia moja kwa moja kwenye Qira’a na baada ya Qira’a Al-hamdu na sura na baada ya hapo unaingia moja kwa moja kwenye Rukuu,namna hiyo.Hivyo haitakiwi kutoa Takbiratul-Ihram kisha kukaa kama dakika tano kama haupo kwenye swala kisha ndio usome Al-hamdu na sura kisha baada ya kurukuu unakaa kama dakika zako kumi ndio unaamua kurukuu,namna hiyo utakuwa hujafatanisha vitendo ktk swala,bali kwa kuachanisha vitendo namna hiyo maana ya swala inapotea kabisa na utatoka nje ya swala na kubatilisha swala yako.Na hataka kusoma sura ndefu kama vle suratul-baqara ukiig’ang’ania mpaka uimalize hatua hiyo inaondoa kabisa ufuatanishaji wa vitendo ktk swala,na ndio ikawa ni bora kusoma sura fupi ktk swala kwa kuzikamilisha na sio nusu yake.

DHIKRI KTK RUKUU

Ukiwa ktk Rukuu,umenyoosha mgongo wako,na macho yako yametizama sehemu ya kusudu, unatakiwa kusoma dhikri hii: “SUBHANA RABIYAL-ADHIMI WABIHAMDIH” (سبحان ربِّيَ العاظيمِ وَبحَمدِهِ) mara moja,au kama hujasoma dhikri hiyo basi usome:SUBHANALLAHI (سُبحانَ اللهِ) kwa kurudia mara tatu na sio chini ya hapo au zaidi ya hapo.

DHIKRI KTK SAJDA:

Ukiwa katika Sajda,katika hali ya utulivu,huku viungo vyako saba vya sajda vikiwa vimegusa ardhini,unatakiwa kusoma dhikri hii: SUBHANA RABIYAL-A’ALA WABIHAMDIH” (سبحان ربِّيَ الأعلی وَبحَمدِهِ) mara moja,au au kama hujasoma dhikri hiyo basi usome:SUBHANALLAHI (سُبحانَ اللهِ) kwa kurudia mara tatu na sio chini ya hapo au zaidi ya hapo.

DHIKRI KATIKA TASHAH-HUD

Katika swala,ndani ya Rakaa ya pili na mwisho wa swala,inatakiwa baada ya Sajda ya Rakaa ya pili mwenye kuswali akae,na akiwa ktk hali ya utulivu wa mwili,asome Tashah-hud kama ifuatavyo:

ASH-HADU ANLA-ILAHA ILLAH LLAH WAHDAHU LA SHARIKA LAHU,WA ASH-HADU ANNA MUHAMMADAN ABDUHU WARASULULLLAH,ALLAHUMMA SWALLI ALA MUHAMMADIN WA A’LI MUHAMMAD.

أشهدُ أن لا إله إلا اللهُ وَحدَهُ لا شَرِيک لهُ وأشهدُ أنَّ محمَّداً عبدُهُ وَرَسُولُهُ اللهُمَّ صلِّ علی محمَّدٍ وَ آل محمَّدٍ.

Huo ndio mwisho wa Tashah-hud ktk rakaa ya pili baada ya Sajda,hapo utatakiwa kusimama kwa ajili ya kuleta rakaa ya tatu,na kama swala yako ni ya rakaa mbili basi baada ya tashah-hud hiyo utatakiwa kufuatisha Salam (AMBAYO NDIO HATUA YA MWISHO WA SWALA YAKO) kama tutakavyoiona hivi punde.

DHIKRI KTK SALAM

Mwenye kuswali,anatakiwa katika Rakaa ya mwisho ya swala yake,na baada ya kusoma Tashah-hud,atoe salam na baada ya salam hiyo swala yake itakuwa imefikia mwisho.Na ambacho ni wajibu ktk salam hiyo-(au tuseme:Sehemu ya wajibu ktk salam)-anachotakiwa kukisoma bada ya kusoma tashahhud hii

(أشهدُ أن لا إله إلا اللهُ وَحدَهُ لا شَرِيک لهُ وأشهدُ أنَّ محمَّداً عبدُهُ وَرَسُولُهُ اللهُمَّ صلِّ علی محمَّدٍ وَ آل محمَّدٍ.) ni kama ifuatavyo:

“ASSALAM ALAINA WA ALA IBADILLAH SWALIHINA, ASSALAM ALAIKUM WARAHMATULLAH WABARAKATUH”.

(السَّلام علينا وعلی عباد الله الصَّالحين،السَّلام عليکُم ورحمة اللهِ وبرکاته). 

Hiyo ndiyo salam ya wajibu ktk swala,lakini ni mustahabu kabla ya salam hizi mbili utangulize salam salam hii ifuatayo:

“ASSALAM ALAIKA AYYUHAN-NABIYYU WARAHMATULLAH WABARAKATUH”:

(السَّلام عليک أيُّها النَّبيُّ ورحمةُ اللهِ وبرکاتهُ).

Hivyo kwa ujumla (ukichukua sehemu ya wajibu ktk salam pamoja na salam hii ambayo ni mustahabu) salam utaianza namna hii kama ifuatavyo:

 {ASSALAM ALAIKA AYYUHAN-NABIYYU WARAHMATULLAH WABARAKATUH,ASSALAM ALAINA WA ALA IBADILLAH SWALIHINA, ASSALAM ALAIKUM WARAHMATULLAH WABARAKATUH}.

(السَّلام عليک أيُّها النَّبيُّ ورحمةُ اللهِ وبرکاتهُ). (السَّلام علينا وعلی عباد الله الصَّالحين،السَّلام عليکُم ورحمة اللهِ وبرکاته). 

Na hapo swala yako itakuwa imeisha,na baada ya kumaliza swala yako,ni mustahabu useme: ALLAH AKBAR” mara tatu.

Salam ni sehemu ya swala,na swala haitimii ispokuwa kwa kuelekea Qibla ,kwa maana kwamba mwenye kuswali anatakiwa kuhakikisha mwili wake na uso wake vyote vimeelekea Qibla anapokuwa kwenye swala, mwanzo wa swala hadi mwisho wa swala.

Kwa mantiki hiyo ikitokea akapinda na kukiacha Qibla,au akageuza uso wake kutoka Qibla na kuuelekeza sehemu nyingi,kulia au kushoto,basi swala yake itakuwa batili.Hivyo basi,maadam tayari mwenye kuswali kaisha ingia kwenye swala kwa kutoa Takbiratul-Ihram,basi anahesabiwa kuwa yuko tayari ndani ya swali ambapo ni lazima azingatie (muda wote akiwa ktk swala) kuelekea Qibla mwanzo hadi mwisho wa swala.

Na tumesema mwisho wa swala ni salam,kwa maana kwamba salam nayo ni sehemu ya swala,imo ndani ya swala,hivyo hutakiwi kuitoa salam pasina kuelekea Qibla,kama ambavyo hutakiwi kutoa Takbiratul-ihram (ambayo ndiyo mwanzo wa swala) kwa kutoelekea Qibla. 

Hivyo,ile kutoa salam kwa kugeuza shingo kulia na kushoto,inahesabika umetoka ktk Qibla,na kutoka ktk qibla kunabatilisha swala,hivyo salam ktk swala inatolewa ktk hali ya kuelekeza uso Qibla.Na ieleweke wazi kwamba sio wajibu wala sio mustahabu kugeuza shingo kulia na kushoto unapokuwa unatoa salam.

Na anakosea anayesema kuwa salam si ktk swala,bali salam ni katika swala kama ilivyo Takbiratul-Ihram,Rukuu,sujuud tahshah-hud,kama ambavyo Rukuu au Takbiratul-ihram au Sujud ….hutakiwi kuitoa pasina kuelekea Qibla kadhalika Salam,hutakiwi kuitoa pasina kuelekeza uso wako Qibla.Na tumesema ni Mustahabu ukimaliza swala yako:Kutoa Takbira kwa kurudia mara tatu,narudia tena: Ni mustahab (na sio wajib) utoe TAKBIR mara tatu ukisema: ALLAH AKBA (الله أکبر).

Mwisho

 

 پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni