Mafunzo ya jamii

MAUMIVU YA KICHWA AU KUUMWA KICHWA

  • Habari NO : 402075
  • Rejea : abna

Si uongo kusema kua hakuna katikajamii hajawahi kusibiwa na ugonjwa huu, lakini ugonjwa huu bado hujafahamikakatika jamii na wengi hadi sasa kuto fahamu sababu za ugonjwa huo, na vipitunaweza kujilinda na ugonjwa huu na mengi zaidi.Maumivi ya kichwa au kuumwakichwa nini?Ugomjwa huu ni ugonjwa ulozagaakatika jamii na hauchaguwi umri au miaka, huwasibu Watoto wachanga, akina Babana akina Mama.Sababu za ugonjwa:1-Uturi(Mafuta uzuri): Rehe kaliya uturi husababisha kuuma kichwa, kama maji ya karafuu kali, Shampoo, eneolililopuliziwa uturi na sabuni ya rehe kali na mengineyo...2- Njaa: Miongoni mwa sababuzinazosababisha kuuma kichwa ni njaa na mlo usokuwa kamili wa kila siku, aukutopata mmoja kati ya mlo wa kila sku, pia ni kutokana na upungufu kiwangokadhaa wa sukari katika baadhi ya miili dhaifu.3-Kutopata usingizi: maumivu yakichwa au kuumwa kichwa aghlabu na mara nyingi husababishwa na kutolala aukutopata mapumziko kama ipasavyo, au yaweza kuwa ni sababu ya kulala kupitakipimo.4- Hli ya hewa: Ubadilikaji wahali ya hewa ni moja kati ya sababu zinazosababisha kuumwa kichwa.5- Kutokuwa na utulivu: Moja katiya sababu za maumivu ya kichwa ni kutokuwa na utulivu kutokana na sababu kadhaazilizosababisha kutokea hali hiyo, kutokua na utulivu husababisha kufikiriasana na kupelekea ubongo kutowa rutuba na hizo rutuba kuwa sababu za maumivu yakichwa.Hivyo basi  tujitahidi kutotumia uturi kupitia kipimo hasazenye harufu kali, tujitahidi kupata chai ya asubuhi na mlo wa usiku tusikosekwani chai na mlo wa usiku ni muhimu zaidi katika kufanya kazi viungo vya mwili,na maneno haya pia yamepokelewa katika baadhi ya hadith za Mtume(saw) kuwa niMakruhu(hairuhusiwi bila kuwekewa mkazo) kutokula usiku, tujitahidi kupumzikawastani bila kuzidisha masaa manane kwa kila siku, tujitahidi pale tutunapojihisi kuwa na uchovu fulani haraka tupumzike kwa muda wa nusu saa au kwalisaa limoja, ama kwa wale wasokuwa na utulivu yategemea maisha yake aishi vipini mwenye familia au la, kama ni mwenye familia ajitahidi kuongea na familiayake ili kutatua tatizo lilokuepo kwani hali ya kutokuwa na utulivu aghlabukatika jamii husababishwa na kazi tunazofanya kila siku kama hatukuzifaanikishahutokea hali hiyo, kwa wasokuwa na familia wajitahidi kuongea na washauri waoili kupata utatuzi wa tatizo lake.Sababu za kuumwa kichwa si hizotu bali ni nyingi ila muhimu ni hizo tulozitaja hapo awali, la muhimutujitahidi kuwa salama na afya njema kwani kuwa na afya njema shughuli zetu zakila siku zitakwenda vizuri bila dosari.


Mourining of Imam Hossein
پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni