Siku ya Arafa

  • Habari NO : 641973
  • Rejea : abna.ir
Brief

Siku ya Arafa ni siku ya tisa ya mwezi wa Dhulhaj, siku hii ni siku ya muhimu sana kwa waislamu hasa kwa Mashia,

Siku ya Arafa ni siku ya tisa ya mwezi wa Dhulhaj, siku hii ni siku ya muhimu sana kwa waislamu hasa kwa Mashia, kwani licha ya fadhila na ubora wa siku ya Arafa, siku hii pia inasadifiana na tukio la Imam Husein (imamu wa tatu wa Mashia) kuanza safari yake ya kuelekea Karbalaa baada ya kuwa amemaliza amali za Hijja, safari hii ndio ilikuwa safari yake ya mwisho kwani hatima ya safari yake ilikuwa ni kuuawa kwake.
Arafa ni neno la kiarabu lenye maana ya (ustahamilivu,utiifu na ufahamu) inasemekana kuwa siku hii imeitwa Arafa kutokana na waja kukili kwa utiifu na kuomba msamaha na toba kutokana na makosa yao.
katika siku hii mahujaji mahujaji hushinda kwenye jangwa la Arafa na kufanya ibada na dua mbalimbali na kisha wanaelekea sehemu inayoitwa Mash-ar ili siku ya Idi iwakute wakiwa katika sehem iitwayo Minaa.
Uislamu unasisitiza watu ambao wahakubahatika kwenda Hija, kufunga katika siku ya Arafa ili wawe katika Ibada kama wale walioshinda katika jangwa la Arafa wakifanya Ibada.
Katika siku hii unaushauriwa kufanya mambo yafuatayo:
- Kuoga josho maalamu kwa ajili ya siku ya Arafa.
-Kusoma ziara ya Imam Husein na kumtakia rehema na Amani Mtume Muhammad s.a.w na kizazi chake kitukufu.
-Baada ya sala ya Alasiri, unatakiwa kusoma dua ya Arafa, kisha kusali rakaa mbili na kukiri na kuomba msamaha, Mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako, na wazazi wako.


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky