jamhuri ya kiislamu ya Iran
-
Jeshi la Iran Lathibitisha kuendelea kutoa Msaada wa Kimkakati kwa wana Harakati za Uhuru za kuyakomboa Mataifa yao dhidi ya Ukoloni na Ukandamizaji
Hatua hii ya Iran inaashiria msimamo wake thabiti katika kuhimiza uhuru na kuunga mkono harakati za kupinga ukandamizaji wa kigeni na ukoloni duniani kote.
-
Kiongozi wa Mapinduzi katika hotuba ya televisheni kwa taifa la Iran:
''Umoja wa Kitaifa wa Iran ni ule ule wa Tarehe 13 Juni 2009; Wote wanawajibika''
Mheshimiwa Ayatollah Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, usiku huu katika hotuba ya televisheni akiwahutubia watu, aliueleza umoja na mshikamano wa kudumu wa taifa la Iran kuwa ni ngumi ya chuma juu ya kichwa cha adui.
-
Je, ilikuwa sahihi kutumia vijana baleghe wachanga katika Vita vya Kulazimishwa (Vita vya Iran na Iraq)?
Nchi kadhaa za Ulaya, ikiwemo Ujerumani, zimeruhusu kisheria ajira ya zaidi ya watoto askari 1,500 chini ya utaratibu wa kipekee wa jeshi.
-
Mkuu wa Majeshi: Vikosi vya Ulinzi vya Iran Vitatoa Jibu Kali Zaidi ya Mawazo ya Wavamizi
“Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na kwa mwongozo wa Kiongozi Muadhamu Ayatollah Imam Khamenei (Mwenyezi Mungu amlinde), vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran viko tayari kugeuza tishio lolote kuwa fursa ya kustawisha nguvu za taifa na kuinua hadhi ya Iran katika mizani ya kimkakati ya kikanda na kimataifa. Jibu letu kwa maadui litakuwa la wakati, kali, la kuumiza na zaidi ya walivyowahi kufikiria.”
-
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Lalaani Mauaji ya Kinyama ya Wazayuni Dhidi ya Yemen-Laahidi Jibu Kali kutoka kwa Muqawama wa Kiislam
"Kinyume na matarajio ya Wazayuni na waungaji mkono wao, jinai hizi hazitaweza kudhoofisha irada ya mapambano ya wananchi wa Yemen, bali damu ya mashahidi hawa watukufu itachochea zaidi hasira na mwamko wa upinzani dhidi ya ukoloni na utawala wa Kizayuni kote katika eneo".
-
Jeshi la Iran:
"Majibu ya Iran yatakuwa makali zaidi iwapo adui atafanya kosa”
Jeshi Kuu la Iran lilibainisha kuwa katika tukio la kosa la kimahesabu kutoka kwa adui, kile kilichozuia operesheni kubwa wakati wa vita vya siku 12 vilivyopita hakitarudiwa tena.