Main Title

source : parstoday
Ijumaa

4 Juni 2021

15:09:29
1147518

Kiongozi Muadhamu: Jamhuri ya Kiislamu ni ubunifu muhimu zaidi wa Imam Khomeini (MA)

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema taifa la Iran hii leo na katika mustakabali wa mbali linapaswa kulinda kumbukumbu ya Imam Khomeini, Mwenyezi Mungu amrehemu.

ABNA24 : Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameyasema hayo leo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi moja kwa moja kwa njia ya televisheni kwa mnasaba  wa kukumbuka mwaka wa 32 wa kuaga dunia Imam Ruhullah Khomeini MA, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ayatullah Khamenei amesema ubunifu mkubwa zaidi wa Imam Khomeini ni Jamhuri ya Kiislamu.

Kiongozi Muadhamu ameongeza kuwa,  kazi kubwa aliyofanya Imam ni kubuni fikra na nadhari ya Jamhuri ya Kiislamu na kuingiza nadharia hiyo katika uga wa siasa na hatimaye kutekeleza nadharia hiyo kivitendo.

Ameongeza kuwa, katika mifumo mbalimbali ambayo imeundwa duniani katika kipindi cha takribani karne mbili zilizopita, hakujashuhudiwa mfumo ambao umetabiriwa kusambaratika kama ilivyotabiriwa kuhusu Jamhuri ya Kiislamu. Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, tokea baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, wale waliochukizwa na mapinduzi hayo walikuwa wanatabiri kuwa yataanguka au kusambaratika baada ya miezi miwili n.k.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa mitazamo kama hiyo ilitokana na uzoefu wa mapinduzi yaliyotokea katika maeneo mengine ambayo yalianza kwa nguvu lakini yakawa na mwisho mbaya.

Ayatullah Khamenei amesema siri ya kubakia na umashuri Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni maneno mawili, Jamhuri na Kiislamu, yaani wananchi na Uislamu. Amefafanua zaidi kwa kusema maana ya Jamhuri ni wananchi, na maana ya Uislamu hapa ni mfumo wa Kiislamu unaotegemea kura za wananchi. 

Ayatullah Ali Khamenei ambaye hotuba yake imerushwa mubashara katika televisheni ya taifa, ameashiria sisitizo la Imam Khomeini la udharura wa kushiriki kwa wingi wananchi katika chaguzi mbalimbali hapa nchini, na kusema kuchagua mtu anayefaa na sahihi ndio suluhisho la mapungufu na matatizo mbalimbali. Ameeleza nukta muhimu zinazohusiana na udharura wa Rais ajaye wa Jamhuri kutekeleza uadilifu wa kijamii, kupambana ipasavyo na bila ya huruma na ufisadi na kuimarisha uzalisha na akasema kuwa: Wananchi wa matabaka yote wanapaswa kushiriki katika uchaguzi na kuwahamasisha wenzao kufanya hivyo.

Vilivile ameashiria kipindi cha awali cha baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini na jinsi mabeberu wa kimataifa walivyokuwa wakitabiri kusambaratika mapinduzi hayo katika kipindi cha miezi miwili, 6 au mwaka mmoja na kusema: Kusimama kidete kwa Imam Khomeini, misimamo yake imara, ushindi mkubwa wa taifa katika vita na masuala mengineyo, yote hayo yalibatilisha utabiri wa mabeberu. Ameongeza kuwa baada ya kuaga dunia hayati Imam Khomeini maadui walikariri matarajio yao hayo ya kusambaratika Jamhuri ya Kiislamu. 

Ayatullah Khamenei ameashiria pia maendeleo na ustawi endelevu unaoshuhudiwa hapa nchini na kusema: Siri ya kubakia hai mfumo wa Imam Khomeini ni kuendelea kushikamana ka mambo mawili yaani Jamhuri (yani wananchi) na Uislamu. 

Kiongozi Muadhamu ameongeza kuwa, miongoni mwa kazi kubwa zilizofanywa na Imam Khomeini ni kubuni fikra ya Jamhuri ya Kiislamu na kuingiza fikra hiyo katika nadharia za kisiasa za kimataifa na hatimaye kutekeleza nadharia hiyo kivitendo.

Amefafanua zaidi kwa kusema kuwa maneno mawili ya "Jamhuri"  na "Kiislamu" kwa maana ya utawala wa Uislamu na wananchi, ndio ufunguo wa matatizo yote na kuongeza kuwa: Wakati wote wananchi wanaposhirikishwa na vigezo vya Uislamu vikazingatiwa, tulipiga hatua za maendeleo; na pale majawapo kati ya mawili hayo halikuzingatiwa na kuchungwa, tulikwama na kutuama. 


342/