Main Title

source : Parstoday
Jumanne

30 Aprili 2024

16:54:17
1455336

Wapalestina zaidi ya 8,500 wametiwa nguvuni Ukingo wa Magharibi tangu Oktoba 7 hadi sasa

Jumuiya ya kushughulikia mateka wa Kipalestina imetangaza katika ripoti yake kwamba utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel umewatia nguvuni Wapalestina 8,505 katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan tangu tarehe 7 Oktoba 2023 mara baada ya kutekelezwa operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa.

Askari wa jeshi la Israel na walowezi wa kizayuni kila siku wanawaua au kuwajeruhi na kuwaweka kizuizini kwa visingizio tofauti wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina. Kwa mujibu wa ripoti Jumuiya ya kushughulikia mateka wa Kipalestina Wapalestina 12 walikamatwa katika Ukingo wa Magharibi katika muda wa saa 24 zilizopita. Tangu tarehe 7 Oktoba 2023, utawala ghasibu wa Kizayuni ulianzisha mauaji makubwa ya kimbari katika Ukanda wa Ghaza dhidi ya watu wasio na ulinzi na madhulumu wa Palestina kwa uungaji mkono kamili wa nchi za Magharibi.Kimya cha jamii ya kimataifa na taasisi za haki za binadamu kwa jinai za utawala ghasibu wa Israel, kimesababisha kuendelea kuuawa wanawake na watoto wa Kipalestina katika vita vya kinyama vilivyoanzishwa na utawala huo haramu.

 Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa tangu Oktoba 7, 2023 hadi sasa, Wapalestina 491 wameuawa shahidi katika maeneo tofauti ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Na kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza, idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi katika katika eneo hilo kutokana na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni tangu Oktoba 7, 2023 hadi sasa imefikia watu elfu 34,488 na idadi ya waliojeruhiwa imefikia elfu 77,643.../

342/