Main Title

source : Parstoday
Jumanne

30 Aprili 2024

16:58:01
1455343

Wanachuo wanaoitetea Palestina Marekani watiwa nguvuni Texas, wasimamishwa masomo Columbia

Polisi nchini Marekani wamekabiliana na wanafunzi wa chuo kikuu katika mji wa Austin jimboni Texas, na kuwakamata makumi ya watu baada ya kubomoa mahema yaliyowekwa kupinga na kulalamikia vita vya kinyama na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ghaza.

Utiaji nguvuni wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Texas huko Austin (UT Austin) umetokea jana wakati Chuo Kikuu cha Columbia jimboni New York City kimeanza kuwasimamisha masomo wanafunzi baada ya kukaidi amri ya kutawanyika. Wanachuo wanaoandamana na kukusanyika kwenye kampasi za vyuo vikuu vyao wanautaka uongozi wa vyuo ukate uhusiano na Israel, ambayo baadhi ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanasema inafanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina huko Ghaza, ambako hadi sasa Wapalestina wasiopungua 34,488 wameshauawa shahidi.Maandamano hayo yamesambaa na kupamba moto katika vyuo vikuu kote nchini Marekani, huku idadi ya waliokamatwa ikikaribia 1,000 wakati siku za mwisho za masomo zikikaribia kumalizika.

 Maandamano ya wanafunzi wanaounga mkono Palestina katika vyuo vikuu vya Columbia na Texas ni mawili tu kati ya mikusanyiko kadha wa kadha ya vyuo vikuu inayoendelea kote nchini Marekani, ikiwemo ya Yale, Chuo Kikuu cha George Washington na Chuo Kikuu cha California, Los Angeles, ambayo kukandamizwa kwake na vyombo vya usalama kwa mkono wa chuma kumeibua masuali kuhusu uhuru wa masomo na uhuru wa kujieleza katika nchi hiyo inayojinasibu kuwa kinara wa uhuru wa watu binafsi na demokrasia.../

342/