Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki amebainisha haya jana katika mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa nchi hiyo Ankara akiwa na mwenzake wa Indonesia, Retno Marsudi.
Katika mazungumzo hayo huko Ankara pamoja na mambo mengine, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki na Indonesia wamejadili na kubadilishana mawazo kuhusu Palestina na hali ya mambo ya Ukanda wa Gaza.
Fidan ameongeza kuwa anatumai kuwa kwa mchakato huu uliowasilishwa katika mahakama ya ICJ mambo yote yatakwenda katika mkondo sahihi. Amesema kwa muda mrefu Uturuki imekuwa ikifanya kila iwezako ili kukubaliwa ombi lake la kujiunga katika kesi hiyo iliyofunguliwa na Afrika Kusini ambapo utawala wa Kizayuni umetuhumiwa kwa mauaji ya kimbari dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki ameongeza kuwa Ankara itaendelea kuwa pamoja na wananchi wa Palestina katika hali zote."
342/