Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

3 Mei 2024

14:12:06
1455924

Trump: Nikichaguliwa kuwa Rais nitarejesha marufuku ya Waislamu kuingia Marekani

Donald Trump mgombea anayetarajiwa kuteuliwa na chama cha Republican kuwania kkiti cha urais nchini Marekani amesema kuwa, akichaguliwa atarejesha tena marufuku ya kusafiri kwa baadhi ya nchi zenye Waislamu wengi katika siku ya kwanza ya utawala wake mpya.

Trump mwenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu, akiwa madarakani, aliweka marufuku ya kusafiri kuingia Marekani kutoka nchi saba zenye Waislamu wengi duniani.

Uamuzi huo ulizua maandamano na changamoto za kisheria, ikijumuisha kutoka taasisi ya American Civil Liberties Union.

Marufuku ya kusafiri Waislamu kwenda Marekani ilikuwa sehemu yenye utata katika muhula wake wa kwanza kama rais na ilibatilishwa na Rais Joe Biden alipoingia madarakani.

Joe Biden alifanya kampeni dhidi ya marufuku ya kusafiri ya Trump mnamo mwaka 2020 na kukomesha marufuku hiyo alipokuwa rais.

Sasa miaka minne baadaye, Trump amewaambia wafuasi wake huko Wisconsin wiki hii kwamba, matukio katika Mashariki ya Kati yanamsadikisha kwamba ni wakati wa marufuku nyingine ya kusafiri.

Donald Trump alipowania urais mwaka wa 2016, aliahidi kubadilisha uhamiaji wa Marekani ili kuwazuia wale aliiwaita kuwa ni magaidi kutoka nchi za Kiislamu.

Katika kampeni zake, Biden ametetea michango ya wahamiaji kwa Marekani, akiliambia kundi la wafadhili wa kampeni wiki hii kwamba nchi zingine zimeteseka kwa sababu zinachukia wageni.

Kura ya maoni ya mwezi Aprili ya Harvard CAPS-Harris inaonyesha kuwa uhamiaji na mfumuko wa bei kama masuala makuu kwa wapiga kura wa Marekani.

Uchaguzi wa Rais nchini Marekani umepangwa kufanyika Novemba mwaka huu.