Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

6 Mei 2024

16:27:39
1456589

Vyombo vya habari Iraq vimekatazwa kutumia jina 'Israel', vinauita 'Utawala wa Kizayuni'

Vyombo vya habari vya Iraq vimeacha kutumia neno "Israel" kumaanisha utawala wa Tel Aviv na badala yake vinatumia msamiati "Utawala wa Kizayuni" katika hatua ya kuonyesha mshikamano na Wapalestina kwa miezi kadhaa sasa.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kamisheni ya Vyombo vya Habari na Mawasiliano ya Iraq (CMC). Ali Almuayid amesema katika mkutano na ujumbe wa vyombo vya habari vya Iran mjini Baghdad kwamba kutumia neno 'Israel' kumepigwa marufuku katika vyombo vya habari vya Iraq; na badala yake magazeti na vyombo vya utangazaji vimetakiwa vitumie msamiati 'utawala wa Kizayuni' au 'utawala ghasibu wa Kizayuni'. Almuayid amefichua kuwa, kumekuwepo na shinikizo kutoka Marekani na baadhi ya nchi nyingine kuzuia uamuzi huo, lakini hivi sasa hatua hiyo imetambuliwa rasmi kuwa ni halali kisheria na inatekelezwa nchini Iraq. Mkuu wa Kamisheni ya Vyombo vya Habari na Mawasiliano ya Iraq allitangaza uamuzi huo mara ya kwanza mwezi Januari kutokana na matukio ya Ukanda wa Ghaza na vita vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya eneo hilo lililowekewa mzingiro, ambavyo hadi sasa vimeshasababisha vifo vya watu wapatao 34,600.

342/