Sanders ameyasema hayo katika ujumbe alioandika kwenye mtandao wa kijamii wa X na kueleza kwamba, kuwaunga mkono watu wa Ghaza na kupinga sera za utawala wa Rais wa Marekani Joe Biden za kuuunga mkono kwa kila hali utawala wa Israel, mara hii kumeanzia kwenye matabaka tofauti ya wanafunzi katika vyuo vikuu vya Marekani. Zaidi ya watu 2,000 wametiwa mbaroni hadi sasa tangu yalipoanza maandamano ya kupinga vita vya kinyama na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza, maandamano ambayo yanafanyika kwa anuani ya "Vuguvugu la Mshikamano na Ghaza", yaliyoanzia katika Chuo Kikuu cha Columbia mjini New York na kuenea kwenye vyuo vingine vya Marekani.Maandamano hayo ya upinzani yameibuka kutokana uungaji mkono wa kila hali unaoonyeshwa na serikali ya Biden kwa Israel na mauaji ya mtawalia yanayoendelea kufanywa na jeshi la utawala huo dhidi ya Wapalestina wa Ghaza.
342/