Joseph Borrell ameeleza hayo kwenye ujumbe alioandika kwenye mtandao wa kijamii wa X, ambapo sambamba na kusisitiza kuwa utawala wa Israel unapaswa uachane na mpango wa kufanya mashambulizi ya ardhini dhidi ya Rafah, amesema Umoja wa Ulaya na Jamii ya Kimataifa zinapaswa kuzuia uvamizi na mashambulizi ya utawala wa Israel mfanyamauaji ya kimbari.Jeshi la Kizayuni limetangaza kuwa, wakazi wa mashariki mwa Rafah wanapaswa kuuhama haraka sana mji huo na kuhamia kwenye lilichokiita eneo "pana la huduma za kibinadamu" la al-Mawasi huko Khan Yunis ili operesheni ya ardhini ya utawala wa Kizayuni katika mji wa Rafah ipate kuanza.
342/