Main Title

source : Parstoday
Jumatano

8 Mei 2024

17:50:48
1457174

Misri: Jamii ya kimataifa imeshindwa kuzuia mashambulizi ya Israel katika mji wa Rafah

Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri amesema kuwa jamii ya kimataifa imeshindwa kuzuia mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza. Sameh Shukry ameeleza haya katika mazungumzo na Mjumbe Maalumu wa Ufaransa katika Masuala ya Lebanon.

Shirika la habari la Uturuki la Anatoli mapemam leo limearifu kuwa, Sameh Shoukry Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri amefanya mazungumzo na Jean Yves Le Drian Mjumbe Maalumu wa Ufaransa katika Masuala ya Lebanon na kutahadharisha kuhusu hali mbaya ya mambo huko Ukanda wa Gaza. 

Shoukry aidha ameyatolea wito mataifa na vyama mbalimbali kudhihirisha msimamo madhubuti na athirifu na yasijiwekee ukomo katika kutoa taarifa na kuwasilisha maombi yao kuhusu Gaza. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wachambuzi na weledi wa masuala ya kisiasa wa Misri wameitaka jamii ya kimataifa kuchukua misimamo mikali na madhubuti dhidi ya Tel Aviv kwa kukiuka mapatano ya kusaka amani na makubaliano ya Philadelphia; na kuzitaja hatua za utawala huo kuwa tishio kwa usalama, maslahi na uongizi wa Misri. 

Weledi wa masuala ya kisiasa wa Misti wamebainisha haya katika hali ambayo wanajeshi wa utawala wa Kizayuni jana Jumanne kwa mara ya kwanza waliingia katika Mhimili wa Philadelphia baada ya miaka 19.  Kwa mujibu wa makubaliano ya maridhiano kati ya Misri na utawala wa Kizayuni ya mwaka 1979, Mhimili wa Philadelphia au Salah al-Din unachukuliwa kuwa eneo la kingo kati ya mpaka wa pande hizo mbili na kuna masharti na viwango vilivyoainishwa kwa ajili ya kuvuka kutoka katika ardhi za Palestina hadi Misri. Katika makubaliano hayo ya maelewano imeelezwa kuwa, iwapo kutajiri hatua yoyote katika mhimili huu tajwa, Misri itapeleka idadi kubwa ya vikosi vyake ili kuhakikisha usalama wake kwa kuzingatia itifaki iliyosainiwa na Tel Aviv. 

342/