Main Title

source : Parstoday
Jumatano

8 Mei 2024

17:55:51
1457182

Bahamas yaitambua rasmi Palestina kama nchi

Wizara ya Mambo ya Nje ya Bahamas imetangaza rasmi kuwa inaitambua rasmi Palestina kama nchi.

Bahamas ni nchi inayojumuisha zaidi ya visiwa elfu tatu vikubwa na vidogo, vilivyoko katika Bahari ya Atlantiki mashariki mwa Florida ya Marekani na kaskazini mwa Cuba. 

Shirika la habari la ISNA limerpoti kuwa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Bahamas imetangaza katika taarifa yake kuwa serikali ya nchi hiyo inaamini kwamba kutambuliwa kwa taifa huru la Palestina kunaonyesha kikamilifu dhamira ya Bahamas kwa kanuni zilizowekwa kwenye Hati ya Umoja wa Mataifa na haki ya mataifa ya kujitawala, ambayo imejumuishwa katika Haki za Kisiasa (ICCPR)) na kubainishwa katika Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni (ICESCR). Wizara ya Mambo ya Nje ya Bahamas imeongeza kuwa: Bahamas ambayo ni nchi iliyopata uhuru wake mwaka 1973 inaunga mkono kikamilifu haki ya kisheria ya wananchi wa Palestina ya kujiainishia uhuru na mustakbali wao wa kisiasa na kufuatilia ustawi wao wa kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Mamlaka ya Ndani ya Palestina imetoa taarifa ikikaribisha na kuunga mkono taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Bahamas kuhusu uamuzi uliochukuliwa na serikali ya nchi hiyo wa kuitambua rasmi nchi ya Palestina na kusema: Inathimini na kushukuru hatua ya nchi hiyo ya kutetea haki ya wananchi wa Palestina ya kujiainisha mustabali wao. Itakumbukwa kuwa mwezi uliopita, Jamaica na Barbados pia zilitangaza kuwa zinalitambua taifa la Palestina. Nchi iliyounga mkono kutambuliwa kwa taifa la Palestina katika wiki za hivi karibuni ni "Trinidad na Tobago" inayopatikana katika Bahari ya Caribbean huko kaskazini mwa Amerika ya Kusini.

342/