Kiwango hicho kikubwa cha joto kimeshuhudiwa licha ya kudhoofika kwa El Nino; wimbi la hali ya hewa ambalo hupasha joto Bahari ya Pasifiki na kusababisha ongezeko la joto duniani. Mwezi Aprili mwaka huu ulikuwa na ongezeko la joto la nyuzi 1.58. Ingawa kuna mabadiliko ya hali ya joto yanayohusiana na mizunguko ya asili kama vile El Nino; lakini imeelezwa kuwa nishati ya ziada iliyonaswa ndani ya bahari na angahewa ambayo huongeza viwango vya gesi chafu itaendelea kusukuma joto la dunia kuelekea rekodi mpya. Haya yameelezwa na Carlo Buontempo wa Taasisi ya The Copernicus Climate Change Service.
Hii ni katika hali ambayo wastani wa halijoto katika kipindi cha miezi 12 iliyopita ulivuka kiwango muhimu cha ongezeko la joto cha 1.5C (2.7F) kilkichoainishwa katika Mtakaba wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Paris 2015.
Mwaka 2015 karibu serikali 200 duniani zilisaini makubaliano hayo ili kuondoa matumizi ya nishati ya fosili itakayochukua mbadala wa nishati katika nusu ya pili ya karne.
\342