Main Title

source : ABNA
Jumatatu

6 Januari 2020

20:58:26
1000004

Msanii marufu wa Sinema nchini Marekani amsuta Trump kwa kuonyesha video ya mazishi ya kamanda Qasim suleimani+ picha

“Robert De Niro” msanii maarufu wa Hollywood amesambaza video ya mahudhurio ya mamilioni ya Wairani walioshiriki kusindikiza mwili wa kamanda Qasim Soleimani iliofanyika katika mji wa Ahwaz, huku msanii huyo akikemea vikali mauaji hayo yaliofanywa kwa amri ya Rais wa Marekani Donald Trump.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mauaji ya kigaidi na kikatili yaliofanywa na Trump pamoja na utawala haramu wa Israel ya kuwauwa kishujaa Kamanda Jemedali Qasim Suleimani, kamanda Abumahdi Almuhandisi na waliokuwa waambata wao, tukio hilo kutokana kutisha kwake limepelekea kukemea suala hilo hata kwa wamarekani wenyewe dhidi ya maamuzi ya serikali yao kwa kufanya tukio hilo la kikatili.
“Robert De Niro” msanii maarufa wa sinema za Marekani, amekemea vikali mauaji hayo kwa kusambaza video ya mahudhurio ya mamilioni ya watu waliosindikiza miili ya makamanda hao katika mji wa Ahwaz nchini Iran.
Msanii huyo akifafanua Video hiyo ameandika: haya ni maadhimisho ya mazishi ya Suleimani katika mji wa Ahwaz, nchini Iran. Inavyoonekana Trump hajafahamu nini amekifanya (kwa kumuuwa Kamanda huyu).



Kusampazwa kwa Video hiyo inayoonyesha mahudhurio makubwa ya wananchi wa Ahwaz, kwa upande mwingine katika mji wa Tehran wamejiteka wananchi zaidi ya waliokuwa wamejitokeza katika mji wa Ahvaz katika kuusindikiza miili ya mashujaa hao waliouwawa kikatili ya shambulio liliofanywa na ndege za marekani mjini Baghdadi.