Shirika la habari AhlulByt (a.s) ABNA: Kama ambavyo katika ujumbe huo ameashiria kwa ukali mno baadhi ya sifa ambazo kiongozi huyo wa Marekani anasifika nazo kama vile dhulma, mabavu na nyinginezo, huku akiashiria kwamba hivyo havitamsaidia pindi atakapoamua kuviwekeza tena nchini Iraq.
“...Kumbuka kwamba nyumba yako ni dhaifu kuliko hata ya buibui, na sauti yako yenye kututisha ni yenye kukera zaidi ya sauti ya punda...” aliandika Sadr.
Haya yamekuja baada ya Rais wa Marekani Bw Donald Trump kutishia kuiwekea vikwazo Iraq ikiwa tu itafanyia kazi mswada wake wa kuyatoa kinguvu majeshi ya Marekani nchini humo.
mwisho/290