Main Title

source : ParsToday
Jumanne

7 Januari 2020

08:36:32
1000146

Bintiye Shahidi Soleimani: Jina la Haj Qassem Soleimani linawatia kiwewe Wazayuni, Wakufurishaji na Mabeberu

Bintiye Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema: "Baba yangu aliwakosesha usingizi madhalimu wote, madikteta na wakufurishaji. Jina la Haj Qassem Soleimani sasa pia linawatia kiwewe Wazayuni, wakufurishaji na mabeberu."

(ABNA24.com) Akihutubia mamilioni ya waombolezaji walioshiriki katika sala ya maiti ya baba yake na mashahidi wenzake katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran, Zainab Soleimani amesema Luteni Jenerali Qassem Soleimani alikuwa na hamu kubwa ya kufa shahidi.

Aidha amewahutubu maadui wa Uislamu na Iran na kusema baba yake alikuwa mpigana jihadi ambaye kutokana na hamu yake ya kufa shahidi alikuwa anafika katika mstari wa mbele kukabiliana na maadui.

Akibainisha zaidi kuhusu jihadi ya baba yake, Bi. Zainab ameendelea kusema: "Katika kipindi cha zaidi ya miaka 40, baba yangu alifanya jitihada zisizo na kikomo na alikuwa na hamu kubwa ya kufa shahidi na alipigana kwa ushujaa na maadui wa Uislamu na ubinadamu."

Aidha bintiye shahidi Soleimani amesema Wamarekani na Wazayuni wafahamu kuwa, kuuawa shahidi baba yake kumeleta mwamko mkubwa zaidi miongoni mwa walio katika mstari wa mbele wa muqawama.

Aidha amesema Wazayuni na Wamarekani wafahamu kuwa  watakumbwa na mustakabali mbaya kwani nyumba zao zinashabihiana na nyumba ya buibui ambayo ni dhaifu na itaangamia tu.

Zainab Soleimani amemhutubu Rais Donald Trump wa Marekani kwa kusema: "Trump, wewe mraibu wa uchezaji kamari, njama yako ya kishetani ya kuibua mgawanyiko baina ya mataifa mawili ya Iraq na Iran itafeli kama ambavyo umefanya kosa la kistratijia la kuwaua Haj Qassem na Abu Mahdi.

"Aidha bintiye Shahidi Luteni Jenerali Soleimani ameashiria hatua ya Bunge la Iraq ya kutaka wanajeshi wa Marekani waondoke nchini humo na kusema: "Familia za wanajeshi wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi zimeshuhudia Marekani ikidhalilishwa vitani huko Syria, Iraq, Lebanon, Afghanistan, Yemen na Palestina na hivyo zisubiri kuangamizwa wanajeshi hao."

..........
340