Main Title

source : ParsToday
Jumanne

7 Januari 2020

08:44:23
1000154

Mamilioni ya Wairani wauaga mwili wa Jenerali Qassem Soleimani na mashahidi wenzake

Marasimu ya kuuaga mwili wa shahidi Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, yamefanyika kwa kuhudhuriwa na mamilioni ya watu mjini Tehran.

(ABNA24.com) Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewaongoza mamilioni ya Waislamu kuswalia swala ya maiti kwa mwili wa Jenerali Soleimani na  Abu Mahdi Al-Muhandis, Naibu Mkuu wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi wa Iraq Hashdu sh-Sha'abi na mashahidi wengine wanne wa Iran ambao waliuawa hivi karibuni katika jinai ya Marekani.

Katika marasimu hayo Kiongozi Muadhamu sambamba na kupongeza juhudi kubwa za mujahidina hao katika njia ya Allah na kupata shahada adhimu, amemshukuru Mwenyezi Mungu na kumhimidi na kuwatakia daraja ya juu mashahidi.

Baada ya swala ya maiti, kulifanyika marasimu ya kusindikiza miili ya mashahidi waliouawa katika jinai hiyo ya hivi karibuni ya Marekani kwa kuhudhuriwa na mamilioni ya watu wakiwemo viongozi wa serikali, wa kijeshi na wa makundi tofauti ya muqawama.

Aidha idadi kadhaa ya mabalozi na wawakilishi wa nchi tofauti wanaoishi mjini Tehran wameshiriki marasimu hayo.

Katika marasimu hayo washiriki wamepiga nara za 'Mauti kwa Marekani,' 'Mauti kwa Israel' 'Hakuna Mapatano Wala Kusalimu Amri, Bali ni Vita na Marekani' 'Mtajuta iwapo Khamenei atatoa hukumu ya jihadi,' kama ambavyo wametaka kulipizwa kisasi kikali kwa hatua ya Washington ya kumuua kigaidi Jenerali Qassem Soleimani na mashahidi wengine.

Leo jioni miili ya mashahidi hao itapelekwa mjini Qum, kwa ajili ya marasimu ya kuwaombea dua na kuwaenzi, huku mazishi yakifanyika Jumanne ya kesho katika mji wa Kerman.

..........
340