Main Title

source : ParsToday
Jumanne

7 Januari 2020

08:48:59
1000155

Ismail Hania ametoka Ghaza kuja Tehran kushiriki maziko ya Kamanda Soleimani; asema Soleimani ni shahidi wa Quds

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ametilia mkazo wajibu wa kuendelea na muqawama hadi ardhi zote za Palestina zitakapokombolewa.

(ABNA24.com) Ismail Hania amehutubia mamilioni ya waombolezaji hapa Tehran na kusisitiza kuwa, mwamko wa muqawama katika ardhi za Palestina utaendelea na mapambano ya kukabiliana na njama za utawala wa Kizayuni na za rais wa Marekani yatazidi kasi hadi ardhi zote za Palestina zitakapokombolewa.

Ismail Hania aidha amesema, Luteni Jenerali Soleimani alipitisha uhai wake wote katika kuunga mkono taifa la Palestina na Kibla cha Kwanza cha Waislamu yaani Msikiti wa al Aqsa na kusisitiza mara tatu kwamba Shahidi Soleimani ni shahidi wa Quds.

Mkuu huyo wa Ofisi ya Kisiasa ya HAMAS aidha amelaani jinai ya Marekani na utawala wa Kizayuni ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Soleimani na kusisitiza kuwa, ushindi wa kambi ya muqawama uliopatikana huko Lebanon na Ghaza bila ya shaka yoyote umetokana na juhudi za Luteni Jenerali Soleimani na bila ya shaka yoyote kambi ya Muqawama itapata ushindi mkubwa pia katika mapambano muhimu mno yajayo.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, Abu Mahdi al Muhandis, Naibu wa Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq al Hashd al Shaabi pamoja na wenzao wengine wanane waliuliwa shahidi usiku wa kuamika Ijumaa tarehe tatu Januari 2020 katika shambulio la anga lililofanywa na utawala wa kigaidi wa Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad, mji mkuu wa Iraq.

...........
340