Main Title

source : ParsToday
Jumanne

7 Januari 2020

08:50:49
1000156

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, usiku wa kuamkia leo amefanya mazungumzo ya simu na Rais Barham Salih wa Iraq na kusisitiza kuwa, ni jambo zito mno kwa mataifa makubwa ya Iran na Iraq kuweza kuvumilia mauaji ya kigaidi waliyofanyiwa Alhaj Qassem Soleimani, Abu Mahdi al Muhandis na wanamapambano wenzao waliokuwa wamefuatana nao.

(ABNA24.com) Rais Rouhani amesema katika mazungumzo hayo ya simu kwamba msimamo wa wazi wa serikali ya Iraq na wimbi kubwa sana la wananchi wa nchi hiyo lililojitokeza katika kuiaga miili ya mashahidi hao watukufu waliouliwa kigaidi na Marekani mjini Baghdad, kumepunguza maumivu ya wananchi wa Iran. Ameongeza kuwa, Iran na Iraq lazima ziimarishe zaidi na zaidi ushirikiano wao wa kukabiliana na uvamizi na uingiliaji wa Marekani wa masuala ya ndani ya nchi hizo.

Rais Rouhani aidha amelishukukru bunge la Iraq kwa kupasisha sheria ya kutimuliwa wanajeshi wa Marekani nchini humo na kuongeza kuwa, ni jambo la yakini kwamba damu za makamanda hao wakubwa wa muqawama zitaleta mabadiliko makubwa katika eneo hili.

Vile vile amepongeza misimamo madhubuti ya wanachuoni na marajii wa Iraq pamoja na ujumbe wa taazia uliotolewa na Ayatullah Sistani kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusema kuwa, ujumbe huo wa Ayatullah Sistan umethibitisha kwamba tunaweza kuendelea na njia hii nzito kutokana na uungaji mkono wa viongozi wakubwa wacha Mungu kama hao.

Kwa upande wake, Rais Barham Salih wa Iraq ametoa mkono wa pole kwa jinai hiyo iliyofanywa na Marekani na kusisitiza kuwa, uhusiano imara, mkubwa na wa kihistoria wa mataifa mawili ya Iraq na Iraq bila ya shaka yoyote una manufaa makubwa kwa eneo hili zima.

...........
340