Main Title

source : ParsToday
Jumanne

7 Januari 2020

08:50:49
1000157

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria kujitokeza mamilioni ya Wairani katika mazishi ya mashahidi wa jinai ya hivi karibuni ya Marekani na kusema: "Uwepo wa kishetani wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi unaelekea kufika ukingoni."

(ABNA24.com) Mamilioni ya wananchi wa Iran leo wameshiriki kwenye shughuli ya mazishi ya Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC na mashahidi wenzake waliouliwa kigaidi na Marekani nchini Iraq.

Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesambaza picha akiwa amejumuika na Wairani katika shughuli hiyo ya mazishi  na kusema: "Donald Trump! Je, katika maisha yako umewahi kuona umati mkubwa kama huu?

Zarif amemhutubu rais wa Marekani na kusema: "Je, ungali unasikiliza vikaragosi vinavyokushauri katika eneo la Asia Magharibi? Na je, ungali unadhani unaweza kuvunja irada ya taifa hili kubwa na watu wake?

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, Ijumaa Alfajiri 3 Januari aliwasili nchini Iraq kufuatia mwaliko rasmi wa wakuu wa nchi hiyo. Punde baada ya kuwasili, akiwa ndani ya gari pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Kamanda wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq maarufu kama al Hashd al Shaabi pamoja na watu wengine wanane, walishambuliwa tokea angani na wanajeshi vamizi na wa kigaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad na wote wakauawa shahidi katika tukio hilo.

..........
340