Main Title

source : ParsToday
Jumanne

7 Januari 2020

08:50:50
1000158

Katibu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika maombolezo ya kukumbuka kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani; Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH kwamba, iwapo Marekani itatekeleza vitisho vinavyotolewa na Trump vya kuishambulia Iran, basi wawe na yakini kwamba miji ya Haifa na Tel Aviv na maeneo mengine muhimu ya Israel yataangamizwa kikamilifu na kusawazisha na ardhi.

(ABNA24.com) Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, Mohsen Rezaee alisema hayo jana hapa mjini Tehran na kuionya vikali Marekani akisema: Marekani ielewe kwamba Qassem Soleimani katika mwili wa taifa la Iran ya Kimapinduzi ni mfano wa Bahman 22, siku yalipofikia ushindi mapinduzi hayo matukufu yaliyotoka ndani kabisa ya nyoyo za Masoleimani wa taifa hili. Amesema, Qassem Soleimani alikuwa mpiganaji jihadi asiyejua kuchoka na katika kipindi chote cha miaka 40 iliyopita alikuwa muda wote katika medani za vita akiyasaidia mataifa manyonge yanayodhulumiwa duniani.

Katibu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aidha amesema, Qassem Soleimani ni shujaa wa tatu wa kimataifa wa Iran baada ya Imam Khomeini na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. Hakuna nukta yoyote duniani katika miaka ya hivi karibuni ambayo haikuwa ikimtaja Qassem Soleimani, hivyo kuuawa kwake shahidi kumeyatia nguvu kubwa Mapinduzi ya Kiislamu na kambi ya muqawama na kumezidi kuonesha sura khabithi na ya kikatili ya Marekani.

Vile vile amesema, Qassem Soleimani alikuwa shujaa katika kambi ya muqawama na alikuwa ni shujaa pia katika mapambano dhidi ya ugaidi hasa hasa ugaidi wa utawala wa Kizayuni wa Israel. 

...........
340