Main Title

source : ParsToday
Jumanne

7 Januari 2020

08:55:14
1000160

Rais Hassan Rouhani ajibu vitisho vya Trump asema: 'Kamwe usilitishe taifa kubwa la Iran'

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa radiamali yake kufuatia vitsiho vya Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu kuyalenga baadhi ya maeneo ya Iran kupitia ujumbe alioutuma kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, ambapo amemuonya kwa kusema: "Kamwe usilitishe taifa kubwa la Iran."

(ABNA24.com) Katika ujumbe huo Rais Rouhani amemuhutubu Trump kwa kumwambia, 'wale ambao wanatishia kuyalenga maeneo 52 yakiwemo maeneo ya kiutamaduni nchini Iran, ni lazima wafikirie pia idadi ya Wairani 290 waliouawa kwenye ndege ya abiria nambari 655IR.'

Ujumbe wa Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unaashiria tukio chungu la kuuawa shahidi watu 290 raia wa Iran katika ndege ya abiria ya nchi hii 655IR hapo tarehe tatu Julai 1988, ambapo jeshi la Marekani lilitekeleza jinai nyingine ya kinyama kwa kuitungua ndege hiyo katika anga ya Ghuba ya Uajemi.

Katika tukio hilo makombora mawili yalivurumishwa kutoka kwenye meli ya kivita ya Marekani ya Vincennes na kuitungua ndege hiyo ya abiria iliyokuwa na abiria 290 wakiwemo wahudumu na watoto 66 pamoja na wanawake 53.

Baada ya kuangushwa ndege hiyo, viongozi wa Marekani na katika kuhalalisha jinai hiyo walitoa sababu za kugongana na kujaribu kulitaja tukio hilo la uhasama dhidi ya Iran kuwa lilifanyika kwa bahati mbaya, hata hivyo kwa kuzingatia meli hiyo kuwa na vifaa vya kivita vya kisasa na mfumo wa rada za computer wa kuweza kubaini aina ya ndege ya abiria iliyokuwa ikipita, ilijulikana kwamba tukio hilo halikufanyika kwa bahati mbaya bali lilikuwa ni katika mwendelezo wa hatua za uhasama za Marekani, dhidi ya Iran ya Kiislamu.

Katika vitisho vyake vya hivi karibuni Trump alisisitiza kuwa iwapo Iran italipiza kisasi kufuatia kuuawa kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, basi Marekani itashambulia maeneo 52 ya Iran yakiwemo ya kiutamaduni, idadi inayokumbushia tukio la miaka kadhaa iliyopita la kuzingirwa ubalozi wa Marekani (pango la ujasusi) mjini Tehran.

.........
340