Main Title

source : ParsToday
Jumanne

7 Januari 2020

08:58:29
1000162

Answarullah ya Yemen: Damu ya Jenerali Qasem Soleimani imeainisha njia ya kuhitimisha uwepo wa Marekani katika eneo

Salim Al-Mughlis, Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa wa Harakati ya Wananchi ya Answarullah ya nchini Yemen amesema kuwa shahidi Qassem Soleimani ameainisha njia ya kuhitimisha uwepo wa Marekani katika eneo hili.

(ABNA24.com) Al-Mughlis amebainisha kwamba kuuawa kigaidi Jenerali Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC pamoja na Abu Mahdi Al-Muhandis, Naibu Mkuu wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi wa Iraq Hashdu sh-Sha'abi mjini Baghdad, Iraq ni jinai na ni lazima kila mpigania uhuru duniani alichukulie suala hili kwa uzito na kuhitimisha uwepo wa Marekani katika eneo.

Salim Al-Mughlis, Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Wananchi ya Answarullah nchini Yemen amesema kuwa ukiukaji wa haki ya kujitawala taifa la Iraq kulikofanywa na Marekani kwa kutekeleza operesheni ya kijinai ya kumuua kigaidi kamanda wa Iran nchini Iraq, ni nukta muhimu kwa muqawama, nayo ni kuongeza mshikamano na harakati zaidi katika kukabiliana na hatari ya Marekani na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Hii ni katika hali ambayo mamilioni ya watu wameshiriki maombolezo ya kuwaenzi mashahidi hao yaani Jenerali Soleimani na Abu Mahdi Al-Muhandis, Naibu Mkuu wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi wa Iraq Hashdu sh-Sha'abi, mjini Sana'a, mji mkuu wa Yemen.

Raia wa Yemen katika mkusanyiko huo wa mamilioni ya watu wamepiga nara za 'Mauti kwa Marekani', 'Mauti kwa Israel' na 'Ushindi kwa Uislamu.'

..........
340